
Wajumbe wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, wakifuatilia mada kuhusu ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi wakati wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dodoma)
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi, WF, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya ametoa rai kwa Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo suala la uwasilishaji wa mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu wa Serikali kwa wakati.
Bw. Mwandumbya ametoa rai hiyo wakati wa kufunga Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.
Bw. Mwandumbya alisema kuwa wajumbe wa Kikao hicho wanatakiwa kusimamia matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki likiwemo suala la matumizi ya control number jumuishi, kufanya kazi kwa weledi bila kutumia mabavu au kukusanya ada na tozo bila kutoa huduma iliyokusudiwa.
Alisema kuwa kwa kufanya hivyo, kutawezesha kuondoa kero na kuweka mazingira mazuri na rafiki ya ulipaji kodi kwa hiyari baina ya walipa kodi.
Kikao hicho kililenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya Kodi ili kuwezesha nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo bila utegemezi mkubwa kwa nchi wahisani.
No comments:
Post a Comment