Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, akikata utepe kuashiria Kuzindua Mradi wa Kuhifadhi Eneo la Historia la Kanisa la Mkunazini Zanzibar, ambalo linabeba historia ya Utumwa Zanzibar kwa kuwa ndipo lilipokuwasokon la kuu la watumwa, akishuhudia uzinduzi huo ni Waziri wa Habari,Michezo, Utamaduni na Utalii Zanzibar Said Ali Mbarouk.uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Filiberto Ceriani, akihutubia baada ya uzinduzi wa mradi huo wa ujenzi wa hifadhi ya sehemu ya historia ya Soko la Watumwa Zanzibar katika eneo la Kanisa la Mkunazini Zanzibar.
Katibu wa Kanisa la Mkunazini Nuhu Justine Sallaya, akitowa maelezo wakati wa sherehe hizo za uzinduzi wa Mradi wa kukarabati eneo hilo la historia ya Zanzibar kupitia Mradi wa Jumuiya ya Ulaya EU.
1 Comments
Hili la kufanyia matengenezo maeneo haya muhimu ni jambo la kupongezwa, lakini juhudi pia itumike kutangaza hapa mkunazini,st monica, ndio ssko kuu la watumwa, na watumwa hawakuuzwa mskiti waijuma malindi, iondoke zana potofu kutoka kwa ndugu zetu watanganyika, kuwa warabu na uislam, ndio ulo uza watu, stmoinca, na mpaka dunia itakapo malizika hapo ndipo palipo kuwa soko na patabaki hivihivo
ReplyDelete