
Mbuyu huu niliupiga picha katika mtaa wa Mkungu Malofa - Chakechake Pemba hivi karibuni.
Ulinikumbusha mengi mojawapo ni kwamba Ubuyu kwa sasa umekuwa ni kitu kimojawapo ambacho ni zawadi kubwa ya tunu kupelekewa wanaoishi ughaibuni.
Na unapotengenezwa kwa kutiwa rangi nyekundu na pilipili manga hupendwa sana na si akinamama pekee sasa mpaka akinababa na watoto. Nasikia ukiupata unaouzwa jaws corner mjini unguja ndio the best. (ni kweli ?...)
Wazungu karibuni ndio kwanza wameugundua na ubuyu umebatizwa kwamba ni Super fruit maana una Vitamin C nyingi sana kupita chungwa mara tano.
Kumbe wazee wetu waliyajua mapema haya nasi tuchangamke kuushughulikia kibiashara zaidi.
No comments:
Post a Comment