Omar Sheha Achukua Fomu
KADA wa Chama cha Mapinduzi na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Omar Sheha Mussa jana, alijitokeza kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Omar Sheha, alichukua fomu hiyo afisi kuu ya CCM iliyopo Kisiwandui ambapo baada ya kuhakikiwa kwa kadi yake na kuwasilisha shilingi milioni moja, Katibu wa kamati ya Itidaki na Uenezi Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimkabidhi fomu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kiembesamaki, alisema kilichomsukuma kuchukua fomu hiyo ni kutaka kuwatumikia Wazanzibari pamoja na kusaidia maendeleo yao ya kiuchumi na kisiasa.
Omar Sheha ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Utawala na Fedha, alisema ana sifa za kuiongoza Zanzibar hasa kutokana na uzoefu wake alionao kwa miaka 30 katika kuwahudumia wananchi wa Zanzibar.
"Mchakato wa kuwania kuteuliwa na chama changu kuiongoza Zanzibar ni hiari yangu binafsi sikushindikizwa na mtu yeyote na si kosa kuomba riadhaa ya kuteuliwa", alisema Mbunge huyo wa Chumbuni.
Aidha alisema kitu cha msingi atakachokisimamia na kuhakikisha kinafanyika endapo atapewa nafasi ya kuiongoza Zanzibar ni kutekeleza kivitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
"Kwa sasa ni vigumu kueleza kila nitakachokifanya endapo nitapewa nafasi ya kuiongoza Zanzibar, ila Ilani ya CCM ndiyo itakayokuwa dira kwenye uongozi wangu", alisema Omar Sheha ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika.
Omar Sheha, alisema pia ana lengo la kuleta mustakbali mwema miongoni mwa wananchi wa Zanzibar pamoja na kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kiuchumi ya Zanzibar.
"Matatizo ya uchumi kwa Wazanzibari nayajua vizuri, tatizo lililopo ni kodi tutazungumza na wenzetu wa upande wa pili wa Jamhuri kuona tunalimaliza tatizo hili na kurejea Zanzibar ya kibiashara".

No comments:
Post a Comment