Habari za Punde

ZANTEL KUZIUNGANISHA SKULI ZOTE ZA MSINGI ZANZIBAR NA HUDUMA YA MTANDAO BURE

Zantel Kuziunganishia Skuli Zote Za Msingi Z’bar Huduma ya Internet Bure



KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel itaziunganisha skuli zote za msingi za Unguja na Pemba katika mtandao wa internet bila malipo katika juhudi zake za kuimarisha huduma za jamii ikiwemo elimu kwa wananchi wa Zanzibar.

Mradi huo utazijumuisha skuli 300 ambapo kila skuli utawalenga wanafunzi wapatao 700 kuanzia darasa la kwanza hadi la nne.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mauzo anaeshughulikia Mashirika wa Zantel, Mohammed Mussa, amesema mradi huo unakuja kufuatia kutiwa saini mradi wa Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano na Usimamizi wa Mfumo wa Taarifa za Elimu katika Maendeleo ya Pamoja ya Elimu Duniani.

Mradi huo unajumuisha makampuni makubwa duniani ya kompyuta na mawasiliano ambayo ni Cisco, Intel na Microsoft, na Zanzibar Telecom Ltd (Zantel) ambayo inajumuika kama kampuni pekee ya ndani ambayo itatoa huduma za mawasiliano ya internet.

Mussa alisema skuli za msingi zitakuwemo kwenye mtandao wa internet bure, ili kurahisisha mfumo wa utoaji elimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.