

Timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zanzibar - Karume Boys - ambayo iko Eritrea kushiriki katika mashindano ya Cecafa katika umri huo imewafundisha soka timu iliyoalikwa kutoka Yemen kwa kuifunga magoli 2 - 1 katika mchezo wa kundi B uliofanyika siku ya Jumapili.
Alikuwa ni kijana Ali Badru aliyefanikiwa kuziona nyavu za Wayemen katika dakika ya 7 na katika dakika ya 24 Karume Boys ilifanya shambulizi la kustukiza lililozaa goli la pili lililofungwa na Ali Othman.
Timu ya Yemen ilijitutumua na kuweza kupata bao katika dakika ya 57 lililofungwa kwa kichwa na Ayman Al Hagri.
Katika kipindi cha pili mchezaji wa Karume Boys, Saleh Hamad alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kutoonesha nidhamu ya uanamichezo na hivyo kuifanya timu kuwa na wakati mgumu kulinda ushindi.
Timu zilipangwa kama ifuatavyo
Yemen: Waleed Mohamed, Ali Nasser, Amr Bawazir (Essam Al-Worafi, dakika ya 48), Yaser Al-Shaiban, Waleed Al-Hubaichi, Mudair Al-Raei (Asaad Al-Reyashi, dakika ya 48), Salem Al-Mouzie, Shehab Sagheer (Ahamed Al-Beidani, dakika ya 66), Eman Tawik, Aiman Al-Hagri, Mohamed Boqshan (Captain).
Zanzibar: Gharib Musa, Makame Hamadi, Said Mussa, Idris Abdulrahim, Salum Said, Is -hak Othman (Ali Othman, dakika ya 46), Ventrous Kamanya (Saleh Hamad, dakika ya 55), Ibrahim Rajab, Ali Juma, Ali Badru, Gharib Musa and Juma Othman.
No comments:
Post a Comment