Habari za Punde

RAIS KARUME AMUWAKILISHA RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WA SADC NCHINI NAMIBIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akiwa ni miongoni mwa Viongozi wa Nchi za SADC akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa siku mbili unaohusu masuala mbali mbali ya Kiuchumi na Kijamii, uliofanyika katika ukumbi wa Safari Court Hotel nchini Namibia,(kushoto) ni Rais wa Afrika Kusini Jacob Gedleyihlekisa Zuma.
Marais wa Nchi Mbali mbali wakisimama wakati wa Wimbo wa Taifa za Nchi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jumuiya ya SADC,uliofanyika Nchini Namibia pia mkutano huo unaadhimisha miaka 30 tokea kuundwa kwa jumuiya hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa Nchi za SADC walioshiriki Mkutano wa Siku mbili uliofanyika Nchini Namibia, katika Ukumbi wa Mikutano wa Safari Court Hotel, Nchini Namibia. Rais karume anamuwakilisha Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Wake za Marais wa Nchi za Jumuiya ya SADC, pamoja na Marais wastaafu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja na washiriki wengine wa Mkutano wa siku mbili wa jumuiya hiyo,wakifuatilia kwa makini, matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Safari Court Hotel

Picha zote na Ramadhan Othman, Namibia

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.