
MGOMBEA Urais kupitia chama cha NRA Haji Khamis Haji akiwahutubia wananchi na wapenzi wa chama chake katika mkutano wake wa kuwania urais wa Zanzibar kupitia chama hicho uliofanyika kiwanja cha kwamabata Magogoni.

WANANCHI wakimsikiliza Mgombea Urais kupitia chama cha NRA Haji Khamis Haji akimwaga sera zake akiwania kinyanganyiro cha Urais wa Zanzibar.

MAKAMO Mwenyekiti wa NRA Simai Abdurahaman akimwaga sera za Chama chake katika mkutano wa kampeni ya kuwania Urais akimnadi Mgombea wake Haji Khamis Haji katika kiwanja cha Kwamabata Magogoni.

WANACHAMA wa Chama cha NRA wakiwa na bendera za chama hicho katika mkutano wa kampeni ya kinyanganyiro Urais wa Zanzibar.

KATIBU Mkuu wa NRA Marshed Humud akitowa sera za chama chake kwa wananchi waliohudhuria mkutano wao wa kampeni ya Urais uliofanyika kiwanja cha Kwamabata Magogoni.

WANANCHI wakisikiliza Sera za Chama cha NRA kikiwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Mgombea wake Haji Khamis Haji

VIONGOZI wa Chama cha NRA wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume na Muasisi wa Muungani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kabla ya kufanya mkutano wao wa kampeni ya Urais wa Zanzibar kiwanja cha Kwamabata Magogoni.

VIONGOZI Chama cha NRA wakiwa na mgombea wao wa Urais kupitia Chama hicho Haji Khamis Haji (katikati) wakisikiliza utenzi katika mkutano wao wa kampeni ya kuwania urais wa Zanzibar kulia Katibu Mkuu NRA Maesheid Humud na kushoto Makamo Mwenyekiti Simai Abdurahman.

MSOMA utenzi Raya Suleiman akisoma utenzi katika mkutano wa Kampeni ya Urais wa Chama cha NRA.

WANAFUNZI wa Madrasa wakisoma kasida katika mkutano wa kampeni wa Chama cha NRA uliofanyika viwanja vya Kwa mabata Magogoni.
Hivi ndivyo mambo yalivyo siku hizi yaani hata kasida zinatumika kwenye majukwaa ya kisiasa?
ReplyDelete