PANDU Ameir Kificho wa CCM, anaendelea kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi chini ya mfumo wa serikali ya Umoja baada ya kumshinda Abbass Juma Muhunzi katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo barazani.
Kificho ameibuka mshindi kwa kupata kura 45 wakati Muhunzi alizoa kura 32 kati ya kura 78 zilizopigwa na wajumbe wa baraza la Wawakilishi.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee alitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika upigaji kura katika Baraza la nane la Wawakilishi na mkutano wa kwanza uliowakutanisha wajumbe wa Baraza hilo uliofanyika Chukwani nje kidogo wa mji wa Zanzibar.
Spika Kificho alipowasili katika ukumbi huo alikula kiapo cha uadilifu kwa kuzilinda na kuzitetea katiba zote mbili ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Mara baada ya hatua hizo, Wawakilishi 79 walikula viapo vya utii na uadilifu kwa kuilinda na kuitetea Katiba ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano Tanzania katika kutekeleza majukumu yao na kumuomba Mungu awasaidie.
Wajumbe hao ni kutoka vyama vya CCM na CUF vilivyoshinda majimbo ya uchaguzi 50 ya Zanzibar pamoja na walioingia viti maalum vya wanawake na walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Wajumbe waliokula kiapo ni Abdalla Juma Abdalla, Abdalla Mohammed Ali, Abdi Mosi Kombo, Abubakar Khamis Bakary, Ali Abdalla Ali, Ali Juma Shamuhuna, Ali Salum Haji, Haji Omar Kheri na Amina Iddi Mabrouk.
Wengine ni Asaa Othman Hamad, Asha Abdu Haji, Asha Bakari Makame, Ashura Sharif Ali, Bihindi Hamad Khamis, Bikame Yussuf Hamad, Farida Amour Mohammed, Fatma Abdulhabib Fereji, Fatma Mbarouk Said, Haji Faki Shaali, Makame Mshimba na Haji Mwadini Makame.
Aidha wajumbe wengine ni Hamad Masoud Hamad, Hamza Hassan Juma, Haroun Ali Suleiman, Hassan Hamad Omar, Hija Hassan Hija, Ismail Jussa Ladhu, Issa Haji Ussi (Gavu), Jaku Hashim Ayub, Jihad Abdillah Hassan, Juma Duni Haji, Kazija Khamis Kona, Mahamoud Muhammed Mussa na Machano Othman Said.
Wengine ni pamoja na Mansoor Yussuf Himid, Mbarouk Wadi Mussa (Mtando), Mgeni Hassan Juma, Mlinde Mbarouk Juma, Mohammed Haji Khalid, Mohammed Mbwana Hamadi, Mohammed Aboud Mohammed, Mohammed Said Mohammed, Mtumwa Kheir Mbarak, Mussa Ali Hassan, Mussa Khamis Silima, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini na Mwanajuma Faki Mdachi.
Wajumbe waliokula kiapo ni Nassor Ahmed Mazrui, Nassor Salim Ali, Omar Ali Shehe, Omar Othman Makungu, Omar Yussuf Mzee, Panya Ali Abdalla, Ramadhan Abdalla Shaaban, Rashid Seif Suleiman, Raya Suleiman Hamad, Rufai Said Rufai, Said Ali Mbarouk, Saleh Nassor Juma, Salim Abdalla Hamad na Salma Mohammed Ali.
Wengine ni Salma Mussa Bilali, Salmin Awadh Salmin, Salum Amour Mtondoo, Balozi Seif Ali Iddi, Shadya Mohamed Suleiman, Shamsi Vuai Nahodha, Shawana Bukheti Hassan, Dk. Sira Ubwa Mamboya, Subeit Khamis Faki, Suleiman Othman Nyanga, Thuwaybah Edington Kissasi, Ussi Jecha Simai, Viwe Khamis Abdalla, Wanu Hafidh Ameir, Zahra Ali Hamad na Zainab Omar Mohammed.
Mapema Katibu wa BLW Ibrahim aliisoma hati iliyosainiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein kuruhusu kuanza kwa Baraza la Wawakilishi la nane, ambapo shughuli kubwa zilizofanyika jana ni pamoja na kufanyika uchaguzi wa spika na kula viapo vya uaminifu kwa wajumbe 79 wa Baraza la Wawakilishi.
Spika wa Baraza hilo, Pandu Ameir Kificho baada ya kukamilika shughuli hizo aliahirisha Baraza hadi kesho, ambapo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein atalizindua na kulihutubia kwa mara ya kwanza.
No comments:
Post a Comment