Habari za Punde

WASTAAFU WAIOMBA SERIKALI KUWATUPIA JICHO

Na Aboud Mahmoud

SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,imeombwa kuwaangalia kwa jicho la huruma wastaafu mbali mbali ambao wametumikia nchi kwa muda mrefu.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (JUWASEJ MUTAZA) Mohammed Ali Maalim wakati wa mkutano wa wanachama hao uliofanyika skuli ya maandalizi Makadara.

Mwenyekiti huyo alisema Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, haina budi kuwasaidia wastaafu hao ili kuondokana na matatizo yanayowakabili.

"Naiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutusaidia sisi wastaafu katika mambo mbali mbali ambayo yatasaidia kujikwamua kimaisha,"alisema.

Mwenyekiti huyo ambae ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Makadara alieleza kwamba lengo na kujikusanya wastaafu hao ni kusukuma mbele maendeleo ya nchi yao.

Alifahamisha kuwa wastaafu hao wana haki na wanahitaji kuthaminiwa kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania.

Jumuiya ya 'JUWASEJ MUTAZA' imesajiliwa Juni 26 mwaka 2009 ambapo kwa sasa ina jumla ya wanachma 506 Unguja na Pemba inahusishwa wastaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Usalama wa Taifa,Hali ya hewa na anga,Wabunge,Jeshi la Polisi na wale wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.