Habari za Punde

DK BILAL MGENI RASMI MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR'AAN DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa fainali za mashindano ya Qur-an kuhifadhi Juzuu 30, zilizofanyika jana Agosti 14 kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Mshindi wa kwanza katika fainali hizo alikuwa ni Mariam Salum Mohamed, kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Aisha Faki Khatib (18), kutoka, Istiqama Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 96 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni  Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Mariam Salum Mohamed (15) kutoka Tarbiyatul-Islamiyah Pemba, aliyeibuka na jumla ya Pointi 97 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gol

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 10 (Tahqeeq), Mohamed Salum (12) kutoka, Darul , aliyeibuka na jumla ya Pointi 98 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa fainali za mashindano ya Qur-an, kuhifadhi Juzuu 30, Shaame Said Shaame(18) kutoka, Ibun Jazary Vikindu, aliyeibuka na jumla ya Pointi 93 katika mashindano hayo yaliyofanyika jana Agosti 14 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, Baraza Kuu la Kiislam (BAKWATA), Shamim Khan, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Al-Haramain jijini Dar es Salaam jana Agost 14. Kulia ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Mkoyo Gole

Picha na Muhidin Sufiani OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.