Baadhi ya vyombo vilivyokusanywa na MUWAZA (jumuia ya Mustakbal wa Zanzibar) na kusafirishwa kutoka Denmark kwa kusudi la kusaidia vifaa fulani vya ICU ya Spitali ya Mnazi Mmoja. Zaidi ya vyombo hivi kuna vitanda 16. Kwa vile Kontena hili lilikuwa limejaa baadhi ya vitu ilibidi vibaki na kusubiri Kontena jengine. Vingi vya vitu hivi vilikusanywa kutoka Spitali ya Kalundborg, na vyengine kidogo kutoka Spitali za Holbaek na Slagelse, zote kutoka Denmark.
DANTAN (Danish Tanzanian Friendship Association) ilisaidia kuomba fedha za kusafirisha Kontena hili. Kurahisisha mapokezi ya Kontena hili ilitumika anwani ya ZOP kwa vile DANTAN tayari ilikuwa na uzoefu wa kutumia anwani hii inapoleta vifaa Zanzibar. Lakini vyombo ndani ya Kontena hili ni mali ya Spitali ya Mnazi Mmoja.
MUWAZA iko mbioni kujaribu kukusanya vifaa tofauti kutoka Denmark, Uingereza na Skandinavia kwa madhumuni ya kuvituma Zanzibar.
Katika juhudi hizi MUWAZA inawasiliana na Ofisi ya Rais ya Daispora ili siku za mbele iweze kutuma vyombo kama hivi ama kwa anuwani ya moja kwa moja kwenye ofisi hio au moja kwa moja na Spitali/ vitengo vitakavyohusika.
Dr. Yussuf S. Salim
Mwenyekiti wa MUWAZA
No comments:
Post a Comment