Habari za Punde

KIKAO CHA PAMOJA SERIKALI YA SMZ NA YA MUUNGANO



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali ya Muungano wa Tanzania kwa Juhudi zake za kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika harakati nzima ya uokozi wa wananchi waliozama katika Meli ya M.M Spice Islanders usiku wa kuamkia tarehe 10/9/2011.

 Balozi seif ametoa pongezi hizo leo asubuhi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Mawaziri wa Serikali za Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichokutana Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam. 


 Balozi Seif amesema Ushirikiano huouliokuwa chini ya vikosi vya ulinzi na usalama vya pande zote mbili za Muungano pamoja na wananchi umepelekea kuokoa maisha ya zaidi ya wananchi mia sita walikuwa wamepatwa na maafa hayo. 

 Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuwasiliana na Afisi ya Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Shimoni Mombasa Kenya kufuatilia miili ya wananchi waliozama kwenye meli hiyo ambapo tayari maiti tano zimeshaokotwa na kufanya idadi ya maiti zilizopatikana kufikia 202. 

 Amesema Wataalamu wa Masuala ya Bahari wameeleza kwamba uwezekano wa kuendelea kuokotwa maiti zaidi katika eneo la Kenya upo kutokana na hali ya bahari na upepo ilivyo hivi sasa. Amewaomba na kuwasisitiza Wananchi kuendelea kupokea Taarifa sahihi za Serikali kupitia vyombo afisi ya Wizara yake ambayo ndio inayowajibika kutoa Taarifa hizo za serikali. “Naweza kutoa Taarifa mimi wakati wote au Waziri wangu wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Rais Mh. Mohd Aboud kufuatia tukio hili. ” Alisema Balozi Seif Ali Iddi. 


Othman Khamis Ame Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 14/9/2011.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.