By Inti,
Kila kitaka yafuta, mengine yanasogea
Chozi churuta churuta, Nguoni yanaingia
Walokufa hawajafata, nasaba nilozaliwa
Wamekufa zinjibari, pahala tulozaliwa
imewabana bahari, hawana pakukimbia
wengi wakitafakari, mauti yanawajia
Mauti ni machungu, hakuna anokataa
huzidi yakiwa chungu, kwa sababu soyofaa
tamaa ya ulimwengu, ndio watu yahadaa
Msiba huu jamani, ukubwa sijaujua
Umeathiri wandani, mpaka nje ya dunia
Roho zetu mefundani, Mola tatuhukumia
Hukumu itapitishwa, wasiwasi tusitia
Mtoto wa miaka sita, baharini aelea
jaketi yeye kavishwa, mama mtu kajifia
nduguye kamkamata, miwili hajatimia
waelea usiku kutwa, macho wazi wakodoa
Nugwi bahari waikata, malaika wawapepea
hapa ndio tunaona, uwezo wa subuhana
watoto hawa wapona, bahari ya maulana
Rabi wape yalomema, duniani na kiyama
Tupoe wazanzibari, msiba ulotufikia
haya si yetu khiyari, tungeweza yazuwia
alipangalo jalali, katu kulipangua
Rabi warehemu, waja walotangulia
Uwatie peponi, moya baada ya moya
huko wende kaonani, na zao familia
No comments:
Post a Comment