Habari za Punde

TANGAZO LA DUA KWA MAREHEMU WA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR

Assalaamu Alaykum.

Kwa niaba ya Watanzania waishio Malaysia kwa kushirikiana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania hapa Malaysia, natoa mualiko rasmi kwa wana ukumbini wote na swahiba zao kuhudhuria dua kwa ajili ya kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki katika ajali ya meli iliyotokea huko Zanzibar hivi karibuni.

Taarifa ya shughuli ni kama ifuatavyo:

Siku na Tarehe: Ijumaa tarehe 16/9/2011
Mahala: Msikiti mkuu wa IIUM (Sultan Ahmad Shah Mosque)
Wakati: Kuanzia mara tu baada ya swala ya Ijumaa.
Utaratibu: Mara tu baada ya kumalizika swala ya Ijumaa, pataswaliwa janaza ghaib itakayoongozwa na Imam wa msikiti. Baada ya hapo watu waliohudhuria kwa ajili ya dua hii wataendelea na kisomo na dua kama ilivyo ada.

Kushiriki kwenu kwa wingi ndio mafanikio ya shughuli hii.

Tunatanguliza shukrani kwa ushirkiano wenu.

Salaam.
Dr. Kassim
IIUM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.