Maiti nyengine tano za ajali ya meli ya Spice Islanders wamepatikana eneo la Shimoni Mombasa na kulazimka kuzikwa kwenye eneo hilo kutokana na hali zao.
Kwa mujibu wa taarifa wa balozi mdogo wa Tanzania nchini Kenya Yahya Haji Jecha amesema kuanzia jana maiti zimeanza kupatikana eneo la shimoni Mombasa.
Amesema kati ya maiti hizo nne ni za wanaume na moja ni ya mwanamke ambapo maiti hizo zimedaiwa kuwa zimeharika sana ambazo zisingeweza kusafirishwa
Katika hatua nyingine kazi za uokozi za kuipata miili mingine kutoka kwenye meli ya Spice Islander iliyozama mwishoni mwa wiki huko Nungwi imesitishwa kwa muda kutoka na hali mbaya ya hewa.
Taarifa kutoka Nungwi zinasema wapiga mbizi wa ndani na wale kutoka Afrika ya kusini wamesitisha kwa muda shguhuli za uokozi kutokana na bahari kuchafuka.
Wakati huo huo usafiri wa baharini kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam umetatizika kutokana na vyombo vya usafiri kuwa kidogo baada ya kutokea ajali ya meli ya Spice Islander.
Hata hivyo nauli za vyombo hivyo zimeripotiwa kupanda maradufu.
Sasa jamani, hivyo watu wameshikwa na msiba nchi nzima na wenye vyombo vya baharini wanazidisha nauli mara dufu? Hivyo kweli huko kwetu kuna ubinaadamu. Kwani ni ktu gani kilichoongeza gharama za usafiri kupandishwa. Je mafuta yamepanda bei kwa sababu ya ajali, je mishahara imepandishwa kwa wafanyakazi wa melini kutokana na ajali, je kuna factor gani hasa iliyowafanya wafanya biashara za usafiri kuwapandishia watu nauli, katika kipindi hiki kigumu. Watu wenyewe hata zaka hawatoi na ndiyo maana kila mara wanapata hasara.
ReplyDeleteKutoka Canada
Ni Paparazi
Yaani mamlaka kama hazipo vile...! sijui hata kama hiyo DNA aliyoagiza rais itafanyika kwa hizo maiti zilizookotwa Mombasa!
ReplyDelete