Amesema ALLAH (SW) “Na tutakujaribuni kwa kila jambo kutokana na khofu na njaa na kupungukiwa mali na nafsi na mazao basi wabashirie wenye kusubiri.Ambao inapowapata misiba husema: HAKIKA SISI NI WA ALLAH NA HAKIKA KWAKE NI MAREJEO”.
(2:155-156).
Umoja wa wanafunzi wa Zanzibar nchini Sudan kwa huzuni wanaungana na wazanzibari wenzao katika kipindi hiki kigumu cha msiba uliolikumba taifa letu.
Tunachukua fursa hii kuwaombea dua ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki. Na wale waliopo mahospitalini ALLAH awaponyeshe kwa haraka na awape subra na awatie nguvu wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Hakika huu ni msiba uliotugusa sote Wazanzibari,Watanzania na Waislam wote duniani.
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA WABARIKI VIONGOZI NA RAIA WAKE.
AMEEN.KATIBU MKUU-ZASU.
YUSSUF A. ALI
No comments:
Post a Comment