Habari za Punde

WAZIRI HAMAD ATEUA WAJUMBE WA BODI BANDARI, SHIRIKA LA MELI NA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amefanya uteuzi wa wajumbe mbali mbali wa bodi ya wakurugenzi katika taasisi za shirika la bandari, shirika la meli na mamlaka ya usafiri baharini.

Uteuzi huo umekuja baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kutangaza wenyeviti wa bodi hayo hivi karibuni.


Mh Hamad Masoud amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Shirika la bandari Zanzibar.

(1) Bw Ali Mohammed Shoka

(2) Bw Salum Toufiq Ali

(3) Bw Seif Said Issa

(4) Bw Omar Haji Omar


Na Bw Ramadhani Nyonje Pandu.

Waziri pia amewateua wajumbe wa bodi ya shirika la meli ambao ni -:

(1) Bw Jecha Thabit Kombo

(2) Bw Ali Ali Hassan

(3) Bw Jabir Hamza Mwalim

(4) Bw Zubeir Ali Maulid

Na Bi Fauzia Mwita Haji.

Aidha Waziri amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa bodi ya mamlaka ya usafiri baharini

Aliowateuwa ni:

Capt Hamza Makame Omar
Bw Hamad Bakar Hamad
Bw Nassir Ali Juma
Bw Shaaban Ramadhan Abdallah
Na Bi Fatma Mohammed Omar

Uteuzi huo umeanza jana baada ya bodi hizo kumaliza mda wake wa miaka mitatu.

1 comment:

  1. Tunaomba picha na profiles zao.Nna wasi wasi kama wanasiasa ni wengi kuliko wataalamu! tena wengine wameshajichokea ..ilimradi tuu!"You can't teach an old dog new tricks" wengine ndio hao walio tufikisha hapa tulipo!...Mungu ibariki ZNZ uipe watu wenye mawazo mbadala.Ukweli ni kwamba "Beautiful ones are not yet born"

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.