Mwenyekiti wa jumuiya ya Aly Amin Society ya Zanzibar Bw, Omary Saleh ikishirikiana na taasisi ya DICC ya Nchini Yemen yenye tawi lake Dar es salaam akimkabidhi msaada wa maafa Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia kuzama kwa meli ya Mv Spice Islanders siku ya tarehe 10/09/2011
Ujumbe wa shirika la ndege la Emirates ulipofika ofisini kwa Makamu wa pili wa Rais Vuga kwa lengo la kukabidhi mchango wao wa Maafa kufuatia ajali ya Mv SPICE
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa msisitizo kwa wananchi kwamba ofisi yake ndio yenye mamlaka ya kutoa taarifa za matukio ya kuzama kwa meli ya Mv Spice ili kuepusha mgongano wa taarifa hizo ambazo zinaanza kuwachanganya wananchi.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
No comments:
Post a Comment