Habari za Punde

TAARIFA ZA KUZAMA MELI - 4

Kwa hapa Nungwi ambapo zoezi hili la uokoaji likendelea wameweza kuletwa watu wapatao sitini wakiwa hai na mpaka ninapoupdate kuna maiti tatu zimepatikana zote za watoto wadogo. 
Kuna Vikosi vya uokoaji vya KMKM pamoja na wakaazi wa Nungwi wakitumia boti zao . Pia Boti za Sea Star na Sea Bus zipo katika eneo la tukio na nyengine zimeweza kuchukua majeruhi na kuwapeleka mjini moja kwa moja viwanja vya Maisara kuweza kutambuliwa na jamaa zao na waliojeruhiwa kupelekwa Hospitalini.

Tutaendelea kuwajuulisha na tukirudi mjini tutaweka Picha. Kama kuna mdau yeyote ana picha au taarifa atutumie kupitia email ili tuweze kuwajuulisha haraka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.