Habari za Punde

TIMU YA TAIFA ZANZIBAR KWENDA MISRI KWA MAZOEZI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar

Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kitafanya mchakato wa kuteua wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar ' Zanzibar Heroes' ambayo itapelekwa nchini Misri kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la Chalenji la CECAFA itakayofanyika jijini Dar es salaam kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.


Afisa Habari Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Munir Zakaria, amesema kuwa kikosi cha timu 
hiyo kitakapokamilika kitaondoka nchini Novemba 1, 2011 kikiwa na watu 30 wakiwemo wachezaji 25 na viongozi wa watano na kitakwenda kupiga kambi kwa muda wa wiki tatu. 

Munir amesema timu ya Zanzibar Heroes, itaweka kambi katika kijiji cha Olimpiki cha Maad kilichopo katikati ya Jiji la Cairo na itacheza michezo nane ya kirafiki na timu za vilabu mbalimbali ikiwemo timu ya taifa ya Olimpiki ya Misri pamoja na miamba Soka ya nchi hiyo ya Zamalek. 

Hii ni mara tano kwa timu hiyo kupiga kambi nchini Misri, ikiwa ni sehemu ya mashirikiano kati ya Zanzibar na Misri, katika mikakati ya kukuza michezo, kubadilishana uzoefu na mbinu mbalimbali za mchezo wa soka. 

Aidha timu hiyo, itarejea nchini kupitia Jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itakayoanza kutimua vumbi Novemba 28, hadi Desemba 10, mwaka huu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.