SERIKALI ya Zanzibar imesema kuwa bado inaendelea kufanya tathmini ya kuwatambua watu halali wanaotakiwa kulipwa fidia kwa waliovunjiwa nyumba zao eneo la Mtoni Kidatu.
Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamhuna aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub, aliyetaka kujua kanma serikali ina mpango wa kuwalipa
wananchi hao na kumtajia idadi ya watu 10 iliyowalipa kama inawatambua.
Akijibu hoja hiyo Waziri huyo alisema bado serikali inaendelea kufanya tathimini juu ya suala hilo ikiwa ni hatua ya kuweza kupata usahihi ni nani anaepaswa kulipwa fidia hiyo.
Alisema ulipaji wa fidia kwa watu hao umeonekana kuwa ni mgumu kutokana na hapo awali serikali ilitoa fedha kuwalipa baadhi ya wananchi hasa waliojenga katika vianzio vya maji lakini watu hao
walirudi kinyemela na kuanzisha ujenzi upya.
Alisema kutokana na hali hiyo alisema serikali sio kama haijui inachokifanya na inalazimika kuwa makini katika kulitekeleza suala hilo.
Naibu Waziri wa Wizara hiyi Haji Makame Mwadini, akijibu suala la msingi la Mwakilishi huyo alisema Wananchi waliovunjiwa Mtoni walilipwa fidia zao ikiwa ni hatua ya kunusuru vyanzo vya maji.
Alisema baada ya serikali kubaini ndipo ilipoamua kuzivunja lakini serikali iliunda Tume kwa ajili ya kuchunguza ni wepi waliostahiki kulipwa fidia kutokana na uvunjwaji wa nyumba hizo.
Alisema Kamati hiyo ilimaliza kazi hiyo na kuiwasilisha serikalini ambayo ilikuwa na mapendekezo ya namna ya malipo yafanyike na anaestahili kulipwa kwa mujibu wa uhalisia wake.
Alisema hadi sasa Wizara hiyo haijatenga kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kufanya malipo hayo hadi serikali itapotoa maamuzi ya muongozo wa namna gani wananchi hao walipwe na ndipo Wizara hiyo
itakuwa katika hali nzuri kujibu hoja hiyo.
Hamna fidia hapo!..hivi bado hamja ielewa serikali yetu?
ReplyDelete