Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI - SERIKALI INAFUATILIA KUTOFAIDIKA WANANCHI NA RASILMALI KISIWA CHA MNEMBA

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi, imesema imo katika hatua ya kulifanyia maamuzi suala la wananchi wa shehia ya Kaskazini ‘A’ wanaodai kutofaidika na raslimali ya kisiwa cha Mnemba.

Kaimu Waziri wa Wizara hiyo, Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Wanawake, Kazija Khamis Kona, alietaka kujua hatua ilizozichukua lkulipatia ufumbuzi tatizo hilo.


Akijibu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Said Ali Mbarouk, Waziri huyo alisema ni kweli serikali inatambua kuwapo kwa tatizo hilo kwa wananchi wa kijiji cha Matemwe, Nungwi, Kijini na Pwani Mchangani na inakusudia kulimaliza.

Alisema katika kulitatua tatizo hilo tayari Wizara hiyo imekaa na uongozi wa Mkoa huo pamoja na muwekezaji anaendesha shughuli zake sehemu hiyo na amekiri kutofanya malipo hayo.

Alisema katika kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kuna makubaliano ambayo yanataratiwa kutolewa maelezo ndani ya mwezi huu na kuwataka wananchi kuvuta sibira wakati serikali ikilishughulikia tatizo hilo.

Adha, waziri huyo alikubaliana na kuwepo kwa tatizo la mkataba waliopewa wananchi kuwa na matatizo baada ya kutokuwa na saini ikiwa ni hoja iliyotolewa na Mwakilishi wa Kiwani Hija Hassan Juma alietaka kujua kama serikali inafahamu kuwapo kwa jambo hilo.

2 comments:

  1. Naona suala hili linataka kupotoshwa maana Wananchi wa Matemwe, Kijini, Pwani Mchangani na Nungwi wamesema hawafaidiki na rasilimali ziliopo kisiwa cha Mnemba.

    Kisiwa cha Mnemba hutembelewa na watalii wasiopungua 50 kwa siku na hutakiwa kila mtalii anayekwenda kustarehe alipe dola 5 za Kimarekani kwa mujibu wa sheria.

    Zamani zilikuwa zinakusanywa na baada ya muda fulani hupelekwa mgao vijijini kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

    Miaka ya hivi karibuni hawapelekewi mgao wao wala hawashirikishwi kwenye maamuzi ndio maana wakaja juu kulalamika maana wanajua pesa zinapofisidiwa

    ReplyDelete
  2. Zaidi ya hayo ya mdau hapo juu, sehemu kubwa ya wafanyakazi wa MNEMBA ISLAND LODGE ni watu wa maeneo yaliyotajwa kua hawafaidiki. binafsi yangu nimejaribu sana kuomba kazi kule ikashindikana. kila umuonae; AME MATI,MADODO FUMU na wengine kama hao. tuweni wakweli.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.