Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI - SERIKALI KUWAPATIA WANANCHI VIFAA MFUMO MPYA WA MAWASILIANO

SERIKALI imesema inatayarisha kuwapatia wananchi vifaa watakavyoweka kwnye televisheni zao kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya mfumo wa mawasiliano kuwa katika Digital

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdilahi Jihad Hassan, aliyasema hayo barazani jana alipokuwa akijibu swali Mwakilishi wa Ziwani, Hemed Rashid Suleiman, aliyetaka kujua serikali kama itawapatia vifaa hivyo ama wananchi wataacha watafute wenyewe.


Waziri huyo alisema serikali imejiandaa kuhakikisha inawapatia wananchi vifaa hivyo na haitawaachia wananchi kuvitafuta wenyewe.

Alisema serikali imo mbioni kukamilisha taratibu za kuingia katika mabadiliko ya mfumo wa mawasiliano ya digitali kwa vile nchi zote za SADC zinatakiwa kukamilisha lengo hilo ifikapo 2012 na sio 2015.


Mapema akijibu suali la Mwakilishi wa Wanawake Mwanaidi Kassim Mussa, aliyetaka kujua hatua ilizochukuliwa na Wizara hiyo kuvibadili katika mfumo wa Digitali vyombo vya habari vya serikali ili visipitwe na wakati, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Bihindi Juma Hamad, alisema serikali imeanza kufanya mabadiliko kwa vyombo hivyo.

Alisema kati ya hatua walizozichukua kwa Televisheni na Redio ni pamoja na kuwaelimisha watendaji, kupata vifaa vya digitali, kuongeza maslahi ya wafanyakazi ili wawe na upendo wa kazi zao.

Alisema madhara ambayo yanaweza kujitokeza ikiwa watashindwa kufanya mabadiliko hayo ni pamoja na kushindwa kuwashawishi walengwa kutizana na kusikiliza vyombo hivyo na kutoipa elimu jamii.

Naibu huyo pia alibainisha hali hiyo ikiwa itaachwa kutokea itaweza kwenda kinyume na maamuzi ya Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) ulioweka muda huo wa kufunga matangazo ya Analogy ifikapo 2015 na pia itakosa ulizi idhaa za serikali pale itapotokea kuingiliwa na idhaa
nyengine.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.