Habari za Punde

KUTOKA BARAZANI - MAWASILIANO YAKIRI HUDUMA ZA AFYA AIRPORT HAZIRIDHISHI

Na Mwantanga Ame

WIZARA ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, imesema huduma za afya zinazotolewa katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, haziko katika kiwango cha kuridhisha kulingana na hadhi ya kiwanja hicho.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ussi Haji Gavu ameeleza hayo katika Kikao cha baraza la Wawakilishi jana wakati akijibu swali la Mwakilishi wa wanawake Mwanaidi Kassim Mussa, aliyehoji kwanini kumekuwa na huduma duni za afya ndani ya kiwanja hicho na kama serikali ina mpango wa kuweka miundombinu ya kituo cha afya katika jengo jipya la uwanja huo.


Naibu Waziri huyo alikiri kuwepo hali isiyoridhisha katika kituo hicho lakini amesema serikali inafahamu hali hiyo na inajiandaa kuhakikisha jengo jipya linakuwa na kituo cha afya bora

Wizara yake italazimika kuona miundombinu hiyo inawekwa kutokana na sheria za viwango katika viwanja vya ndege zimekuwa vinawataka kufuata viwango vya ICAO vinavyowiana na viwanja vya ndege mbali mbali duniani.

Kutokana na kuwepo kwa sheria ya viwango hivyo, Zanzibar inalazimika kuzifuata lakini kwa bahati mbaya ujenzi wa jengo linalotumika hivi sasa katika uwanja huo haukufuata viwango hivyo.

Alisema kutokana na hali ya maendeleo iliopo, yoendelea katika ujenzi mpya wa jengo la kiwanja cha ndege cha Zanzibar ina mpango wa kutenga na kuwapatia eneo linalokidhi kwa ajili ya kituo cha afya hapo jengo litapomalizika 2013.

Naibu huyo akielezea juu ya taasisi ambazo zimepewa kusimamia utoaji wa huduma katika kiwanja hicho alisema ikiwa ni Afya linasimamiwa na Wizara husika na Benki na taasisi za kifedha zinazokubalika baada yakufikia makubaliano maalum,

Aidha, Naibu huyo alitoa wito kwa taasisi za kibenki kujitokeza kutoa huduma katika kiwanja hicho kwa kuzingatia vigezo na miongozo ya kimataifa kuhusu shughuli za utawala na uendeshaji wa huduma katika viwanja vya ndege.

Hata hivyo, alikanusha maelezo ya kukosekana sehemu za kujisaidia kiasi kwamba kuna baadhi ya watumishi wamekosa sehemu na wanajisaidia katika kichochoro.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.