Habari za Punde

UVCCMYATAKA MADARASA YA ITIFAKI YAFUFULIWE

Na Marzouk Khamis,Maelezo Pemba

MWENYEKITI wa Jumuia ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi,Mkoa wa Kusini Pemba Ali Suleiman Juma amesema kazi kubwa inayowakabili viongozi wa Jumuia za Chama Cha Mapinduzi hivi sasa ni kuyafufua madarasa ya itikadi ya chama katika ngazi za matawi na majimbo ili kuimarisha uhai
wa chama.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Vijana Taifa aliyasema hayo katika tawi la CCM Matale alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa tawi hilo ikiwa ni ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na jumuia zake katika jimbo la Chonga.


Alisema kutoendelea kwa madarasa hayo katika ngazi za matawi na majimbo kunawavunja moyo vijana wengi ambao ni tegemeo katika chama na jumuia zake.

Alifahamisha kuwa mchango wa kuwepo kwa madarasa hayo katika uimarishaji wa shughuli za chama ni mkubwa kwani kunawakutanisha vijana na kuwapa fursa katika kuchangia masuala yanayowahusu.

Aidha alisema iwapo vijana watapatiwa mafunzo katika ngazi husika ni dhahiri kuwa watahamasika kujiunga na jumuia za chama pamoja na kushiriki katika nafasi mbali mbali za uongozi.

Akizunumzia kuhusu suala la ajira kwa vijana, alisema hivi sasa ni vigumu kwa serikali kuwapatia ajira vijana wote,lakini hata hivyo serikali inajitahidi kutafuta kila njia kuona vijana wanawezeshwa kwa kupatiwa mikopo kupitia vikundi vya ushirika.

Alisema CCM kupitia Jumuia ya Umoja wa Vijana Tanzania imeandaa mpango wa kufungua Benki za mikopo zitakazotoa mikopo kwa viajana kupitia vikundi vya ushirika hivyo aliwataka vijana kuanzisha vikundi vya ushirika katika matawi ili waweze kufaidika na mikopo hiyo

1 comment:

  1. UVCCM hamuwezi kufanikiwa mpaka mtuombe radhi! Wakati wa 'sekeseke' za kisiasa ZNZ, miaka ya 1995-2010 mliwafitini wengi kati ya vijana wenu, huku mkiwahusisha na upinzani ili iwe rahisi kuwanyima fursa zilizokua zikipatikana wakati ule wa 'ushabik'. Matokeo yake chama chetu mkakidhoofisha na kikabaki kutegemea nguvu ya dola. Kwa vile sasa 'ushabik' umeisha na zile fursa 'kwishne!' wengi kati ya 'wadandia basi' hamuaonekani tena!..sasa mda umefika mkae chonjo, mtuachie wenyewe tuimarishe chama chetu!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.