Habari za Punde

SERIKALI YATILIANA SAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO NA CHUO CHA KILIMO NA UFUNDI CHA FLORIDA - FAMU

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Na Rais Wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Na Ufundi Cha Florida Nchini Marekani Dk.James H. Ammons Wakitia Saini Mkataba Wa Mashirikiano Kati Ya Chuo Kikuu Cha Florida { Famu } Na Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar { Suza }.


Mkufunzi Wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Na Ufundi Cha Florida { Famu } Dr. Leonard Perry Akimuonyesha Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozo Seif Ali Iddi Akionyeshwa Moja Ya Injini Iliyobuniwa Na Wataalamu Wa Chuo Hicho.

Dr. Subramanian Ramakrishnan Akimtembeza Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Katika Moja Kati Ya Maabara Kuu Ya Chuo Kikuu Cha Kilimo Na Ufundi Cha Florida { Famu }.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini Makataba wa Mashirikiano kati yake na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida { FAMUJ } Nchini Marekani.

Mkataba huo una lengo la kubadilishana uzoefu na Utaalamu kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZAZ}.

Utiaji saini huo umefanyika katika Majengo ya Chuo hichocha Florida yaliyopo katika mji wa Tallahassee ambapo kwa upande wa Zanzibar umewakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ule wa Florida umewakilishwa na Rais wa Chuo hicho cha { FAMU } Dr. James ammons.


Akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa pia na wanafunzi wa fani fofauti chuoni hapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameshauri taaluma inayotolewa na chuo kikuu cha Florida iingie katika nchi changa ili kuleta mabadiliko ya kilimo na ufundi.

Balozi Seif alisema Mataifa mengi yanayoendelea hasa yale ya Bara la Afrika bado yanashindwa kukabiliana na changamoto zinayoyabaliki licha ya kwamba Mataifa hayo yanategemea Kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%.
“ Florida University iwe kiungo cha kuunganisha Taaluma katika vyuo vikuu vya nchi changa kikiwemo kile cha suza ”. Alisema Balozi Seif.

Mapema Rais wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi cha Florida{ famu } Dr.James Ammons alisema Chuo hicho kinalenga kujenga nguvu ya Taaluma katika kuona kizazi cha sasa kinapata Elimu inayokwenda sambamba na mabadiliko ya kasi ya Sayansi na Teknolojia Duniani.

Dr. ammons alisema Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 125 iliyopita kimefungua masomo ya Taaluma ya Madawa na Sheria yakianguliwa nay ale ya Kilimo na Ufundi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kukitembelea kitengo cha Ufundi cha Chuo hicho cha Florida { FAMU -FSU }.

Mkuu wa Kitengo hicho cha ufundi Dr. Regional Perry alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake hatua waliyofikia chuoni hapo ya kifanya utafiti katika masuala ya Madawa na Wanaadamu.

Dr. Perry alisema wataalamu wa chuo hicho tayari wamefikia hatua ya kutengeneza Injini za vyombo vya moto.

Othman Khamis Ame

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.