Na Haroub Hussein, Pemba
WAISLAMU kisiwani Pemba wameupongeza uamuzi wa viongozi wa Tanzania kupinga kuridhia ndoa za jinsia moja kama mashatri ya kupewa misaada na nchi ya Uingereza.
Hivi karibuni waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alizieleza nchi zinazoendelea kuwa endapo zisiporidhia ndia za jinsia moja zitarajie kunyima misaada na nchi hiyo.
Mwenyekiti wa jumuia ya Istiqama kisiwani Pemba, Sheikh Mohammed Suleiman alieleza hayo alipokuwa akitoa mawaidha muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya swala ya Ijumaa katika msikiti wa Alhalim, uliopo Chake Chake.
Alisema vitendo vya ndoa za jinsia moja ni vya kulaaniwa, hivyo serikali kutoa msimamo ambao unaungwa mkono na wananchi ni hatua nzuri nay a kupigiwa mfano.
Sheikh Muhammed alisema uamuzi serikali za Tanzania kupinga kuridhia vitendo hivyo kwa masharti ya kupewa misada ni wa kupongezwa na waislamu kwa ndio dini yenye kupinga vitendo hivyo.
Mwenyekiti huyo alisema uamuzi huo wa serikali ni wa kijasiri na wenye kuonesha mfano kuwa mataifa yanayoendelea yana haki ya kukataa yale wanayoamrishwa kama hayana maslahi kiuchumi na kiutamaduni kwa wananchi wao.
Alisema kitendo cha waziri Cameron kutaka nchi wanachama wa jumuia ya madola kutunga sheria za kuwa na ndoa za jinsia moja ni kitendo cha udhalilishaji kwa nchi ambazo haziendani na utamaduni wa aina hiyo.
Aidha aliwataka viongozi serikali za Tanzania kuwa makini juu ya masharti ya kupewa misaada yanayotolewa na na nchi tajiri, kwani mengine ni magumu kutekelezeka kutokana na kutokubalika katika jamii.
Alisema kutokua makini kunaweza kusababisha nchi kuingia katika mitego isiotegemewa ambapo mataifa yaliyoendelea hutumia mbinu hizo na kuziingiza nchi masikini katika migogoro na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.
Sheikh Muhammed, alisema Uislamu unapinga suala la uzinifu sambamba na ndoa za jinsia moja, hivyo aliwataka waislamu kufuata maamrisho ya dini yao ili kuepuka adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Aidha alishauri serikali kueleza wazi wazi kwa nchi mbali mbali wahisani juu kuwa na masharti yanayofuata misingi ya ubinaadamu.
Viongozi kadhaa wamejitokeza kupinga vitendo vya kukubali ndoa za jinsia moja ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alitoa msimamo wa serikali yake juu ya kupinga vitendo hivyo.
Viongozi wengine waliotoa kauli ya kupinga vitendo hivyo ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alisema vitendo vya kuingiliana jinsia moja hata wanyama hawafanyi hivyo haviwezi kuridhiwa na Tanzania.
No comments:
Post a Comment