Habari za Punde

DK BILAL ASEMA LENGO NI KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA

Na Fatuma Kitima, Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal amesema serikali ipo katika mikakati kuhakikisha nchi inazalisha chakula cha kutosha kwa matumizi ya watanzania wenyewe pamoja na kufanya biashara ya chakula nchi za nje.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Dk. Bilal katika ufunguzi wa mkutano wa mpango wa uwekezaji katika kilimo wenye lengo la
kuhakikisha sekta ya kilimo inategemewa kiasi kikubwa katika bajeti za nchi wanachama wa umoja wa Afrika (AU).


Dk.Bilal alisema kuwa serikali itahakikisha nchi zenye matatizo ya njaa zilizopo katika bara la Afrika zinapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa watazalisha mara mbili ya ilivyo sasa.

Dk. Bilal alisema wakati huu serikali ipo katika mchakato wa kuhakikisha inawawezesha wakulima na wafanyabiashara kwa kuwaunganisha na masoko ya kimataifa.

“Nchi yetu imejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika suala zima la kilimo “alisema Dk. Bilal

Wakati huohuo Waziri wa Kilimo na Chakula Jumanne Maghembe alisema hivi sasa kuna chakula cha kutosha katika hifadhi ya ghala la taifa kwa kuwa asilimia 95 ya chakula kinachotumika Tanzania ambapo ni asilimia 5 tu ndio chakula kutoka nje ya nchi.

Hata hivyo alisema serikali imeuza chakula tani 10,000 kwa Wold Food Program na tani 40,000 kwa wafanyabiashara wa Kenya.

Mkutano huo umekutanisha wadau mbalimbali wa kilimo kutoka umoja wa Afrika kwa lengo la kushinikiza bajeti za nchi husika kutenga pesa za kukuza kilimo kutoka asilimia 6 mpaka 10.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.