Habari za Punde

WANAOWAHILIKI WANYAMA KUKIONA

Na Husna Mohammed

SHERIA kwa ajili ya ukatili dhidi ya wanyama iko mbioni kukamilishwa ili kuwatia hatiani watu wanaohusika na ukatili huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya kuzuia ukatili kwa wanyama na utunzaji wa mazingira, Ali Abdalla Juma, alisema rasimu kwa ajili ya urekebishaji wa sheria hiyo uko mbioni katika Idara ya Maendeleo ya Mifugo na mara baada ya kukamilika kwake itatumika.


Alisema sheria iliyopo sasa haina mashiko jambo ambalo linawapa mwanya wafugaji kufanya wanavyotaka dhidi ya wanyama.

Mkurugenzi huyo alizitaja kasoro zilizomo ndani ya sheria hizo kuwa ni pamoja na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mtu aliefanya kosa dhidi ya mnyama kama kumpiga bakora.

“Mahakamani ni lazima kuwepo ushahidi wa kutosha kama alama kwa mnyama na mambo mengine yanayohusiana na hayo”, alisema.

Aidha alisema kuwepo kwa sheria ya ukatili dhidi ya wanyama kwa kiasi kikubwa kutasaidia kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanyama kama kuwapiga sana, kuwaumiza na hata kuwabebesha mizigo kupita uwezo wao.

Abdalla aliwataja wanyama kama punda na Ng’ombe ndio wanaopata mateso makubwa kutoka kwa wafugaji jambo ambalo limekuwa likisababisha mateso makali kwa wanyama hao.

Katika kuwajali wanyama hao, Jumuiya hiyo jana ilitoa chanjo ya wanyama wa aina mbalimbali katika kijiji cha Ndijani Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.