Habari za Punde

BINGWA WA KARATE ZANZIBAR KUSAKWA PEMBA

Na Mwajuma Juma

MASHINDANO ya Kanda ya mchezo wa karate katika staili ya ‘Gojruu’ kutafuta bingwa wa Zanzibar, yanatarajiwa kufanyika kisiwani Pemba Januari 5, mwaka ujao.

Katibu Mkuu wa Chama cha Karate kwa staili ya ‘Gojruu’ Haji Kombo Faki, amesema kuwa michuano hiyo itashirikisha timu zote za Unguja na Pemba.


Alieleza kuwa michuano hiyo itashirikisha timu zote za Unguja na Pemba, yakitanguliwa na maonesho maalumu kuhusu mchezo huo.

Aidha, alifahamisha kuwa, mchezaji atakaeibuka bingwa katika mchezo huo, anatarajiwa kupambana na bingwa wa staili ya ‘Shokhan’.

Kuhusu zawadi, Faki alifahamisha kuwa bingwa atapata kikombe na medali, wakati mshindi wa pili atapewa medali pekee.

Mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Wete kisiwani Pemba, yatakuwa ya siku moja na yatashirikisha wachezaji wanawake na wanaume.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.