Na Mwajuma Juma
MABINGWA watetezi wa Kombe la Taifa la mpira wa mikono timu ya Mwanakwerekwe, inaendelea vyema na kampeni zake za kutetea taji inalolishikilia katika mashindano ya mchezo huo yanayofanyika Potoa
Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mwanakwerekwe iliyoshuka dimbani saa 2:00 za asubuhi jana iliweza kuifunga timu ya Michamvi mabao 33-12, mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka pande zote mbili.
Hadi miamba hiyo inakwenda kupumzika, Mwanakwerekwe ilikuwa mbele kwa mabao 12-3. Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa mabingwa hao, ambapo katika pambano lake la kwanza, walifanikiwa kuifunga Potoa mabao 23-12.
Mbali na mchezo huo, kulifanyika mechi nyengine katika michunao hiyo, ilishuhudia Ndijani ikiifunga Pete mabao 15-13, huku Michamvi wanaume wakailaza Kibuyuni mabao 13-9.
Aidha wenyeji timu ya Potoa, wakaendelea kugawa takrima kwa kukubali kichapo cha mabao 19-17 dhidi ya Michamvi wanawake.
No comments:
Post a Comment