Habari za Punde

USAID LATOA MSAADA WA GARI IDARA YA USTAWI WA JAMII

Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa jamii zanzibar, Halima maulid Salum akijaribu kuliwasha gari hilo baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu, Fatuma Gharib Bilal jana.
Katibu Mkuu Fatuma Gharib Bilal (kushoto) akimkabidhi funguo za gari hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa jamii Zanzibar, Halima Maulid Salum.
Katibu Mkuu Fatuma Gharib Bilal akijaribu kuliwasha baaya ya kukabidhiwa

Charles Matiko (kushoto) akikabidhi funguo ya gari kwa Katibu Mkuu, Fatuma Gharib Bilal
Picha na Martin Kabemba.

Shirika la misaada na maendeleo la Marekani, USAID kupitia mradi wake wa FHI 360 limekabidhi gari aina ya SUZUKI lenye thamani ya sh.milioni 58 kwa ajili ya mradi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Gari hilolenye namba za usajili 8374 lilikabidhiwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa jamii, maendeleo ya vijana, wanawake na watoto, Fatuma Gharib Bilal.

Aliyekabidhi kwaniaba ya USAID, Charles Matiko ambaye ni Project Director, Systems Strengthening Project.

1 comment:

  1. Ni matunda hayo.
    Lakini dada zangu msilitumie hilo gari kwendea maharusini bwawani.
    Litumike kwa walengwa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.