Na Mwanajuma Mmanga
WAFANYABIASHARA wa soko la Darajani wametakiwa kudumisha usafi katika soko hilo ili kuondokana na maradhi mbali mbali ya mripuko yanayoweza kutokea.
Mkuu wa soko hilo Fadhil Khatibu Shaaban alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Darajani Mjini Zanzibar.
Alisema kuwa ni vyema wananchi kushirikiana na baraza la manispaa katika shughuli za usafi kwani ni jukumu la kila mmoja juu ya kuwajibika na usafi huo.
Wakati huo huo mkuu huyo akizungumzia sababu zinazo pelekea kupanda kwa bidhaa mara kwa mara sokoni hapo ni usafirishaji wa bidhaa hizo na matakwa yao binafsi hali inayo wakandamiza wanunuzi mbali mbali wa bidhaa hizo.
Mkuu huyo alizitaja baadhi ya bidhaa zilizo panda sokoni hapo ikiwemo muhogo,mbatata,mananasi nazi na tungule hali ambayo inarudisha nyuma wanunuzi wanao hitaji bidhaa hizo.
Alifahamisha kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakijivutia wao wenyewe katika uuzaji wa bidhaazao bila ya kujali maslahi ya wengine hali ambayo inawakandamiza wanaohitaji kimaisha.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuwa na ustahamilivu juu ya hilo kwani tatizo hilo limekuwa likipigiwa kelele katika vyombo mbali mbali vya habari.
No comments:
Post a Comment