Na Khamisuu Abdallah
WANAFUNZI wa skuli ya Kitongani wametakiwa wajiepushe na makundi maovu na badala yake wajishughilishe na masomo yao kwa bidii hali ambayo itaweka vyema mstakbali wa maisha yao.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui alieleza hayo hivi karibuni huko Kitogani wilaya ya Kusini Unguja kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika skuli ya msingi ya kijiji hicho.
Waziri huyo aliwafahamisha wanafunzi wa skuli hiyo kuacha kujiunga na vikundi viovu vsivyo na maadili na badala yake wajishughulishe na masomo yao kwani ndiyo yatakayowasaidia katika kupata maisha mazuri ya
baadae.
Alisema njia nzuri ya maisha ya baadae kwa wanafunzi hao ni kusoma kwa bidii na kuacha kuwa wanachama wa vikundi vyenye kutumia bangi na dawa za kulevya.
Mazrui aliwataka wanafunzi hao wasome kwa bidii ili waweze kujikimu kimaisha na kuondoka na umasikini kwa kuweza kujenga maisha yao ya baadae kwa kuja kutegemea ajira kutoka serikalini isipokuwa kuja
kujiajiri wenyewe.
Aliwapongeza aliwapongeza viongozi wa jimbo hilo kwa ushirikiano wao na wananchi wao kwa kuanzisha ujenzi wa skuli katika shehia yao jambo ambalo ni zuri na lakupigiwa mfano.
“Napenda kuwapongeza viongozi wa jimbo hili pamoja na wananchi wao kwa kushirikiana na kuweza kufanikisha watoto kwenda masafa marefu kwa kufuata elimu hili ni jambo la kupongezwa”, alisema Mazrui.
Akisoma risala Mwalimu Abubakar Ramadan Ali alisaema changamoto zinazowakabili ni udogo wa eneo la skuli hiyo ambao wanafunzi wanakuwa wanapata tabu wakiwa madarasani.
Kuchelewa kufika walimu skuli kwa kungojea usafiri ambao hauna uhakika ni wa kubahatisha paoja na kituo cha Afya na kukosekana kwa umeme katika skuli hiyo.
Nae Mkurungenzi wa Tasisi ya Karume Sayansi na Tekinolojia Abdul-hamid Idrisa kwa niaba ya katibu mkuu wa Wizara ya Elimu alisema aliahidi kuchukua jukumu la kuwezeka skuli hiyo na kujenga maabara kwa ajili ya wanafunzi ili waweze kwenda na sayasi na teknolojia.
Katika uwekaji jiwe la msingi huo, Mazrui aliahidi kuchangia mifuko100 ya saruji iweze kusaidia katika ujenzi wa skuli hiyo kwa utiaji wa plasta.
No comments:
Post a Comment