Habari za Punde

Dk Shein Akabidhiwa Ripoti ya Michezo ya Mapinduzi Cup

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipokea ripoti ya kamati ya mapinduzi Cup 2012 na Katibu wa Kamati hiyo Khamis Abdulla Said,wakati wa wajumbe wa kamati
hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais.


Mwenyekiti wa Kamati ya wajumbe wa Mapinduzi Cup 2012 Mohamed Raza,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia) wakati kamati hiyo
ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar Kuonana na Rais .
Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,Abdilah Jihadi Hassan,akiwatambulisha wajumbe wa kamati ya Mapinduzi Cup 2012 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,walipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na kamati hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa Mapinduzi Cup 2012 na wajumbe wa kamati ya Kikombe hicho,akiwemo
Mwenyekiti Mohamed Raza (watatu kushoto) baada ya hafla ya kuwazawadia vyeti wafadhili wa mashindano ya mchezo huo, yaliyomalizika hivi karibuni wakati wa Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika
uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar,wakati wa hafla hiyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar jana.

Picha na Ramadhan Othman Ikulu

1 comment:

  1. Hongereni sanaKamati, mulifanya kazi nzuri sana

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.