Habari za Punde

Dk. Shein Ateua Wenyeviti Watatu wa Bodi

Na Mwandishi wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteua Tatu Ali Abdulla kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa uteuzi huo umefanywa chini ya hati ya kisheria (Legal Notice) namba 111 ya mwaka 2011 na
umeanza rasmi Januari 16 mwaka huu.


Aidha Dk. Shein amemteua Dk. Yussuf Nuhu Pandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali.

Uteuzi huo umefanywa chini ya kifungu 14(1) (a) cha sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali namba 10 ya mwaka 2011, uteuzi ambao rasmi umeanza Januari 16 mwaka huu.

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemteua Kassim Maalim Suleiman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC).

Uteuzi huo umefanywa chini ya kifungu namba 13(2)(a) cha sheria ya shirika la Biashara la Taifa namba 11 ya mwaka 2011.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi, uteuzi huo umeanza rasmi Januari 16 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.