Habari za Punde

Kikao cha Baraza Kimeanza Leo

Na Mwantanga Ame

MKUTANO wa sita wa Baraza la nane la Wawakilishi, unatarajiwa kuanza leo, ambapo wajumbe wa Baraza hilo wataanza kwa kipindi cha masuala na majibu.

Taarifa iliyotolewa na Baraza hilo kwa vyombo vya habari Mjini Zanzibar imeeleza kuwa kikao hicho kinatarajiwa kufanyika kwa muda wa kipindi cha wiki mbili.

Alisema katika kikao hicho jumla ya masuala 127 yanayotarajiwa kuulizwa Barazani hapo na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na baadae Watendaji wakuu wa serikali watayatolea ufafanuzi.

Alisema kinatarajia kuipokea miswada miwili ukiwemo wa sheria ya maslahi ya viongozi wa kisiasa ya 2012 na mswada wa sheria ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar ya 2012.

Alisema tayari wajumbe wote wa baraza hilo wameshaarifiwa kuanza kwa kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.