Habari za Punde

WANAFUNZI SITA ZANZIBAR KUSHIRIKI WARSHA UGANDA

Na Mwashamba Juma

WANAFUNZI sita wa michipuo ya sayansi kutoka skuli za Zanzibar wanatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika warsha ya siku 10 nchini Uganda ambayo itashirikisha mataifa saba kutoka Afrika.

Wanafunzi hao wakiwemo wasichana watatu wa kidatu cha tatu kutoka skuli ya sekondari Kiponda, na watatu kutoka skuli ya mchipuo wa biashara Mombasa wa kidato cha tatu wavulana wawili na msichana mmoja wanatarajiwa kuondoka nchini kuelekea chuo kikuu cha Makerere Uganda.


Wanafunzi hao watakaoandamana na mkuu wasafara, Mwalimu Fat-hiya Brek Mohammed ni Maryam Juma Othman, Rawhiya Kasongo Khamis na Rehema Suleiman Mzee wote kutoka skuli ya sekondari Kiponda, Bahati Hamad Ali, Hubayb Said Saleh na Said Omar Fateh kutoka Mchipuo wa biashara Mombasa.

Mwalimu Fat-hiya alisema, semina hiyo itawajumuisha wanafunzi kutoka mataifa saba ya Afrika yakiwemo Tanzania ambayo itawakilishwa na Zanzibar, Kenya, Uganda ambao ni wenyweji katika warsha hiyo,
Botswana, Nigeria, na Afrika ya Kusini.

Aidha, Fat-hiya alisema warsha hiyo imedhaminiwa na mradi wa African Gifted Foundation (AGF) ulio chini ya Uingereza ambao unaongozwa na Archie Mathesom.

Mbali na warsha inayotegemewa katika ziara ya wanafunzi hao, lakini pia wanatarajiwa kutembelea sehemu za kitalii na za kihistoria za nchini Uganda.

Fat-hiya ni mkufunzi advance katika masomo ya kiingereza katika skuli ya sekondari ya Kiponda.

Alisema wanafunzi waliochaguliwa katika warsha hiyo ni wale waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi yakiwemo Hesabati, Phizikia na Kiingereza, ambao walifanyiwa usaili kwa kutakiwa kuandika insha ya
maneno 300.

Mwalimu Fat-hiya aliwahi kushiriki katika programu ya Youth Exchange Studies (YES) program ambayo ilizishirikisha skuli za sekondari 20 zikiwemo 12 kutoka Tanzania bara, 3 kutoka Pemba na 5 Unguja kwa
Zanzibar.

Progamu hiyo iliyotoa mafunzo ya miezi 10 ilisimamiwa na Marekani mwaka 2009.

2 comments:

  1. HONGERENI SANA HAYO NDIO TUYATAKAYO,
    WALIMU JITAHIDINI ,JAPO HALI YA MAISHA NI NGUMU.
    MUNGU ATAWASAIDIA.

    ReplyDelete
  2. Hongera Bi Fathiya. izi programa za Youth Exchange au Studie Exchange ni Project nzuri ambazo zinaweza kuwapatia Elimu ya Marifa, Jamii, na utamaduni Vijana wetu wa Zanzibar ambao ndio taifa la Zanzibar la kesho.

    Kusafiri peke yake ni moja ya elimu, kwani mtu anapotoka nje ya Nchi yake basi huona mambo mengi mazuri na yamaarifa ambayo anaweza kuyaiga.

    Hivyo tunawaomba Walimu Wetu wa School za Unguja na Pemba mujitahidi kusomesha kwa takua ili watoto waweze kusoma lugha za kingeze zaidi kuliko kiswahili. Kama tunavojua Visiwa vyetu ni Vivutio vya Utalii na hili hatuwezi kuliepuka. Lakini Tunataka jamii iweze kutoa wanatoto bora ambao watakua weledu wa lugha za kigeni hasa kingereza. Wao ndio watakoa liongoza Taifa la kesho.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.