Habari za Punde

Mafunzo ya Siku Tano ya Kuulinda Utamaduni wa Tanzania na Zanzibar.

 Kamishna wa Utamaduni Zanzibar Hamad Bakari Mshindo akizindua mafunzo ya siku tano ya kuimarisha utamaduni wa Tanzania kwa Maofisa wa Utamaduni wa Tanzania Bara na Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani.Zanzibar. 
 Maofisa wa Utamaduni wakimsikiliza Kamishna wa Utamaduni Zanzibar akifunguwa mafunzo hayo.
Mkuu wa kitengo cha UNESCO Dar-es-Salaam Program Specialist Culture Sector. Adele Nibona akitowa maelezo jinsi ya Kuimarisha utamaduni wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kusimamia utamaduni wa Tanzania.na kuimarisha maadili.

Baadhi ya Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Kamishna wa Utamaduni Zanzibar Hassan Mshindo.
Culture Expert UNESCO Silverse Lisamula Anami, akitowa maelezo jinsi ya kuimarisha utamaduni na jinsi gani mtu anaweza kuuhishimu utamaduni wa mwezake.


2 comments:

  1. Imekuwaje watu wa bara na Zanzibar kufanyiwa semina moja juu ya utamaduni? Kwani tuna utamaduni sawa? Kuna utamaduni wa Mtanzania kweli.Naomba anaejua anieleweshe.

    ReplyDelete
  2. Sielewi, ukisema bara unakusudia wapi, lkn. kama unatumia ile tafisiri ya hapa kwetu kwamba bara ni upande wa pili wa muungano, nadhani tuna mengi yanayofanana kiutamaduni.

    Kama utakumbuka vizuri, asili ya watu wengi wa Z'ar inasemekana ni washirazi basi ujuwe kua zile jahazi saba za akina Muhsin bin Ali kutoka persia, hazikuja moja kwa moja Z'bar zilianzia KILWA, BAGAMOYO MAFYA NA kwengineko ktk mwambao na ndio mana hadi hii leo kuna magofu ya Washirazi kule KAOLE Bagamoyo.

    Ni kutokana na mfanano huu wa kiutamaduni kuliko fanya BERLIN CONFFERENCE
    iifanye Z'bar kua visiwa vya UNGUJA, PEMBA, MAFYA NA MAILI 10 NDANI YA MWAMBAO KUTOKA MALINDI HADI SOFALA.

    Aidha utamaduni ni pamoja na lugha, dini mavazi nk. na haya yote tunafanana na wenzetu wa mwambao kiasi kwamba baadhi yao hujisikia kua karibu zaidi na sisi kuliko hata hao tunaosema ni wenzao.

    Ni kweli tunatofautiana kiutamaduni na baadhi ya makabila hasa yale yasiokua ya mwambao lkn. nadhani kushirikishwa kwetu ktk hilo kumetokana na sababu nilizi zitaja

    Mm naulizia huyu mwl. wangu HAMAD BAKARI MSHINDO amebadili jina? naona hapa ameandikwa Hassan?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.