Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara Julius Mtatiro,akimtambulisha Mgombea wa Chama cha CUF kwa Wananchi wa Jimbo la Uzini, katika mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Bambi.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Uzini kwa Tiketi ya CUF Salama Hussein Zaral, akitowa sera za Chama chake kwa Wananchi wa Bambi ikiwa ni moja ya Mkutano wake wa Kampeni jimboni humo.
Naibu Katibu Mkuu CUF Zanzibar Ismail Jussa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Uzini, wakati wa mkutano wa kampeni ya Uchaguzi mdogo wa Uzini uliofanyika katika viwanja vya skuli ya bambi.
Mjiumbe wa Baraza Kuu la CUF Juma Duni, akitowa nasaha zake katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa jimbo la Uzini katika viwanja vya skuli ya bambi.
Wanachama wa Chama cha CUF wakishangilia katika mkutano wa kampeni ya jimbo la Uzini.
Wananchi wa Kijiji cha Bambi wakisikiliza sera za Chama cha CUF katika mkutano wa kampeni katika viwanbja vya skuli ya Bambi.
Wanachama wa CUF wakimsikilizxa Mgombea wao akitowa sera za Chama chake.

Tokea amfitinishe Hamad Rashid nikimuona tu huyu Jussa nahisi kichef chefu.
ReplyDeleteNa vifuu tundu wamo tu kuunga mkono. Mm naamini CUF yatakuja kuwakuta yalee.. taliyowakuta HIZBU walipomfukuza katibu mkuu wao Al marhum MOH'D ABDUL RAHMAAN BABU.
Babu aliwaambia pale uwanja wa malindi," mimi natoka lakini, yatawatokeeni mambo ambayo mtakuja kunikunbuka daima"
Aa.. kama.. kawaida kumbe, vifuu tundu hawakuanza leo..wakatiwa bangi na ALI MUHSIN BARWAN, wakashangiria " ah.. kilichotokea!..Ulizeni wazee ..wengine mpaka leo wameishia ughaibuni, wamebaki 'enzi zetu!!