Habari za Punde

Msivunje Muungano : Dk. Bilal

Na John Gagarini, Kibaha

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal amewataka Watanzania wasikubali kuvunja Muungano kwa kupitia marekebisho ya katiba mpya.

Aliyasema hayo jana Mlandizi Kibaha Vijijini wakati wa sherehe za kutimiza miaka 35 za kuzaliwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani na kusema kuwa Watanzania wanapaswa kudumisha Muungano na wasikubali kurubuniwa na wanasiasa wasioitakia mema nchi.


Alisema kuna baadhi ya wanasiasa wanataka kutumia marekebisho hayo kutaka kuvunja Muungano na kuleta Usultani jambo ambalo si zuri kwani Muungano umeleta mambo mazuri mengi na kikubwa kikiwa ni amani iliyopo.

"Kama mtu anakuja kuwaambia kuwa mvunje Muungano kwa kupitia marekebisho ya katiba msikubaliane naye, kwani haitakii mema nchi yetu kwani amani na upendo vimedumu kwa kupitia Muungano hivyo tusikubali kudanganywa," alisema Dk. Bilal.

Dk. Bilal ambaye ni mlezi wa CCM mkoa wa Pwani alisema kuwa watanzania wanatakiwa kutumia uhuru wao vizuri kwani ni kama kisu endapo utatumiwa vibaya unaweza kuleta matatizo lakini ukitumiwa vizuri utaleta mafanikio.

"Pia viongozi wawe makini na kuachana na tabia za kufanya biashara za magendo bali wafanye shughuli halali kwani itaondoa rushwa," alisema Dk. Bilal.

Aliwataka WanaCCM kila mmoja kuwa mwenezi wa habari za mambo mazuri yaliyofanywa na chama katika kipindi chote tangu chama kuanzishwa kwake kwani mengi mazuri yamefanyika katika kipindi hicho.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Abuu Jumaa alisema katika kukienzi chama yeye kama Mbunge kwa kushirikiana na wananchi wake watahakikisha wanatekeleza yale yote ambayo yako kwenye ilani ya chama.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka alisema chama kiko kwenye changamoto kubwa lakini hiyo ndiyo itakayosababisha kupatikana kwa maendeleo kwani bila ya changamoto mambo hayawezi kwenda.

15 comments:

  1. Makamo wa rais hana haja ya kuzunguka sana, wanotaka kuvunja muungano wanajulikana, ni CUF na CHADEMA.

    CUF: wao wanadai kwamba tukiwa nje ya muungano tutapata misaada mingi kutoka nje na hivyo visiwa vitaendelea LAKINI wanasahau kua hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa misaada na kama ni hivyo WAKOMORO leo hii wasingekua masikini.

    Kwa upande wa CHADEMA wao wanadai kwamba Waislamu wa bara wanapata kiburi kutoka Z'bar, hivyo nje ya muungano watajua namna ya kudeal nao.

    Pili wanadai kua Wazanzibari wamejaa sana DSM na wanafaidika na fursa nyingi za kiuchumi zilizopo na hawaishi kulalama, wakati wabara waliopo zanzibar ni masikini.

    Hivyo makamo rais asitafune maneno na awataje tuu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. TOBOWA UKWELI.LAKINI JEE VIZIWI WATASIKIA ?
      MWENYE HASIRA NA CHUKI HASIKII.
      CHUKI DHIDI YA WA BARA NA UBARA NI MARITJI YA JADI
      KWA KUTAKA KUFICHA UDHALIMU WA KALE CHINI KWA CHINI.

      Delete
  2. Wewe makamu wa rais ni mtu uliyesoma tafadhali usiwababaishe watu kwa ajili ya kulinda maslahi yako na cheo chako. Waachilie wananchi waamue wenyewe kwani wao ndiyo wenye nchi wanachotaka au wanaloamua ndilo litakalokuwa. Wewe au kiongozi mwengine mmoja hana haki ya kuwaamulia walio wengi. Tafadhali usijifanye huoni na kufumba macho. Tuambie Faida gani ilizozipata Zanzibar za kiuchumi tokea iingizwe kwenye nakama hii ya muungano zaidi ya umaskini. Hatutaki tena tumeshachoka Zanzibar ilikuwepo kabla ya muungano na itaendelea kuwepo bila muungano. Mtoaji sio wewe wala kiongozi mwenzako. Rizki anayetoa ni Mola na huyo ndiye wa kumtegemea kwa kila kitu. Na bora ungeacha kuwatisha watu bure na fikra zako hizo finyu za kuleta usultani kwani hayo yameshapitwa na wakati sasa watu hawadanganyiki tena. CCM WENZAKO walitumia danganya hizo kuwagawa Wazanzibari ili wapate kuwatawala na kuwanyonya kiuchumi lakini sasa wameshawashitukia na wameamka kwa hiyo hawatodanganyika na maneno yasiyo na msingi kama hayo na mengineyo. Kama huna cha kusema bora unyamaze kimya ndiyo ustaarabu na ndiyo kupata thawabu na siyo kuropokwa.

    ReplyDelete
  3. VOICE OF ZANZIBAR YOUTH
    *MUUNGANO MWISHO CHUMBE* *MUUNGANO MWISHO CHUMBE*


    Tunataka nchi yetu huru tushachoka kutawaliwa na Tanganyika inayojiita Tanzania kwa kiini macho sio.
    wazee wetu mliweza kuwadanganya na kuwatawala na mumewacha na umaskini mkubwa kama sio wa Zanzibari.....Vijana Wa ki Zanzibari wa leo sio wale wa 60s na 70s lijuwe hilo Mzee Harib Bilal..sote tupo kitu kimoja sasa hivi sio sisi tu hapa nyumbani ujue pia na WaZanzibari wote wanaoishi nje ya Zanzibar basi msimamo wao ndio ule ule Free Zanzibar.
    Bilal na wale wengine pia viongozi wa serikali musijaribu kabisa kutudanganya Wa Zanzibari wa leo kwa hilo nakwambieni hamutofanikiwa kabisa....maoni yetu kwenu kutoka kwa "Voice of Zanzibar Youth" TUKILALA TUKIAMKA TUKIENDA Tunawaza vipi tutafanikiwa kuuvunja muungano huu na tuirudishe Zanzibar yetu huru.
    Habari ndio hiyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana na wewe Muungano mwisho Chumbe.Tanganyika kivyake na Zanzibar kivyake kama Zamani.Tukotayari kujitoa muhanga kwa Zanzibar yetu,tushachoka kutawaliwa na Watanganyika kwa kivuli cha Tanzani.
      Mafisadi wakubwa na wezi Hatutaki Muungano.Tulikuwa na kila kitu chetu muungano huu unatutia ufukara.Hatukubali tena kuletewa siasa za Ubaguzi,hakuna CCM wala CUF Uzanzibari kwanza.
      Tutapigania nchi yetu hata kama tukifa sote,atakaebaki aishi katika Zanzibar huru...
      Mungu Ibariki Zanzibar

      Delete
  4. Naunga mkoni hoja, ela uradhi wangu tukiipata jemshid aitwe aje amalize muda wake, walimuonea buree.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jemshid ,alipongolewa kitini 1964 kwa kweli ilimbidi aaende
      kule kwao asiliya Oman/Muscat atawale .Lakini ilishangaza
      kua hajenda huko bali alibaki Uingereza.Aliogopa nini yeye
      kwenda Oman ,kwenye uasili wa Ufalme wa Ukoo Wake ?

      Zanzibar sasa imo mikononi mwa wenyewe kila mtu kwao,wasio
      penda hivyo kila mtu anajuwa asili ya mababu na mababu zao
      nawende huko - Muungano ndio nguvu za Afrika.

      Delete
  5. Visiwani watu wote ni wa kuja , hakuna mtu alichimbuka kwenye kisiwa.

    ReplyDelete
  6. Jemshid hakuweza kurudi tena Oman kwani kulikua na mtawala mwengine ambae pia alikua mfalme. Lakini pia ufamle kwa Jemshid aliupora kutoka kwa Bi Matuka kutokana na kuwa yeye alikua mwanamke hivyo kulikua na sababu kadhaa kwa nini Jemshid asiende Oman naomba ufatilie historia ya Zanzibar japo kwa muhtasari.

    Zanzibar haitaki kujitoa katika muungano ati kwa sababu ya misada peke yake hayo ni miongoni tu hizo muzitazo kero tu za muungano lkn haiwezi kuwa ni ndio sababu kuu ya msingi. Nadhani sababu hasa ni kuwa Zanzibar irudi kama ni sovereighty na uhuru wake kamili kama ni nchi ndani ya muungano na nje ya muungano na bila ya shaka itakua na mamlaka ya kusimamia uchumi wake, ushirikiano wa kimataifa, sheria zake n.k kikamilifu.

    Hata na huko mabara pia wakuja wako wengi sana pengine wewe mababu zako wanatoka Nyasaland walihamia hapo Tanganyika jee waweza jua hivyo? Hivyi kwa nini ishindikane kuelezwa faida za muungano huu. Inasikitisha sana inapotekezea kuwaulizwa ndugu zetu wa bara au wale mateka wao wa [CCM-znz] wakupe faida za muungano ukasikia mijineno kama ya huyu mzee wetu dk Gharib Bilal mara sijui kudumisha amani, mara wapemba wengi wana maduka kule bara..! ni usanii mtupu na mambo ya kipuzi kama hayo ya kurudisha warabu hivi vile.

    Tusome alama na nyakati sio wakati ule tena wa kudanganyana kwa huu muungano wa kitapeli tapeli mie hainishangazi sana kuona hawa watu wa jamhuri kuutetea huu muungano feki kwa sababu unapomtapeli mtu huwa wafanya kila njia kutetea maslahi yako uko tayari kusema lolote la kudanganya danganya ilimradi uzuge wewe yako yakuendee.

    ReplyDelete
  7. Na wewe duniani ni wa kuja tuu, hivyo ami kataa tayari kwenda kwenu. Sasa ikiwa kila mtu ni wa kuja tuu ina maana kila atakaye aje tuu. lete hoja sa msingi wacha maneno ya kitoto.

    ReplyDelete
  8. Unajua huu mzee kashakaribia kufa sasa kwahiyo anaona Munguno ukivungika yeye hatukuwa na cheo tena na anaogopa kutokulindwa tena na mapikipiki sasa mungano ukivungika yeye hana kitu.

    ReplyDelete
  9. Ndugu zangu tupunguzeni jazba!
    tutoe maoni mazuri na ya kistaarabu ambayo yatatufikisha ktk malengo yetu.

    Kwa Z'bar tukianza kubaguana kwa kuambiana, nani mgeni na nani mwenyeyeji naona kama hatobaki mtu hapa!
    Waz'bari wengi ni; Wabantu, warabu,wangazija, wahindi, washirazi, Wagunya nk... haya nambieni nani ktk hawa mwenye asili ya hapa zaidi?

    Jabo lolote ukilifanya kwa jazba hata busara zinakupungua, kwa mfano kuna mtu nasenma eti JEMSHID alipora ufalme kutoka kwa BI MATUKA.
    Jamani aliechukua ufalme kwa BI MATUKA ni SAID KHALIFA(babu mzaa baba wa JEMSHID),na hii ilikua baada ya kumuoa.

    Wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kusema eti muungano hauna faida, huu si ukichaa huu?
    Mimi nakubai matatizo yapo, tena mengi lkn. yanaweza kutatuliwa kwa busara na sio kwa kuvunja muungano..hasa tukizingatia kua mengine yalisababishwa na wazee wetu pengine kwa jazba baada ya warabu 'kuwazingua' au kwa ukosefu wa elimu.

    Lkn.zadi ya yote hayo, hebu tujiulize maswali yafuatayo:

    1) Hivi z'bar kushidwa kujitosheleza sio tu kwa chakula lkn. hata mboga mboga na kuendelea kuitegemea bara ni tatizo la muungano?

    2)Hivi Z'bar kushindwa kusimamia vizuri elimu na kuwaacha watoto wengi wasome DINI na KIARABU na hatimae kushindwa kupata ajira ni tatizo la muungano?

    3)Hivi sisi kushindwa kusimamia vizuri ardhi chache tuliyonayo na kuwaacha watu wajenge ovyo ovyo( bila plani )hili ni tatizo la muungano?

    4) Hivi, kushindwa hata kuhamasisha upandaji miti na hivyo kutufanya tegemezi wa mbao, mkaa na miti ya kuezekea hili nalo ni tatizo la muungano?

    Kumbukeni hata hivo vibiashara tunavovifanya tunategemea sana soko kutoka nje ya hapa ikiwemo bara.
    Kubwa zaidi hapa ni kujenga utamaduni wa kutatua matatizo yetu bila kulaumu wengine, penye matatizo tuseme lakini utamaduni wa mtu kua hajala, kagombana na mkewe ua mtoto wa ke kafeli FORM 11, AKASINGIZIA MUUNGANO sivyo!!

    ReplyDelete
  10. MIMI NAONA TATIZO HAPA NI UTUMWA WA HISTORIA.
    WATU WANAANGALIA VITABU VYA ZAMANI AMBAVYO VINASEMA ZANZIBAR ILIKUA TAJIRI,ILIKUA INATAWALA KARIBIA ROBO YA BARA LA AFRIKA N.K. VIJANA WANAOTA PEMBE!

    LAKINI TUJIULIZE,NCHI ILIKUA IKITEGEMEA NINI KIUCHUMI?
    UTAAMBIWA ILIKUA IKISAFIRISHA WATUMWA, PEMBE ZA NDOVU KARAFUU N.K.
    LA MUHIMU HAPA NI KUKUMBUKA KUA SISI HATUNA TEMBO NA UTUMWA UMEKWISHA,KARAFUU SASA HIVI KILA NCHI INAZALISHA JEE TUTASAFIRISHA NINI?

    INAOSHESHA WENZETU WANATUTAFUTIA MAAFA, YAANI TUTOKE HAPA TWENDE TANGANYIKA TUKANUNUE NGO'MBE, SIMBAURANGA, VIAZI, NA VYENGINEVYO KWA DOLA

    NAJUA HAPA BOKO HARAM NA AL SHABAB WATASEMA, MBONA ZAMANI BASMAT, VITUNGUU SOMI NA MBAO VILITOKA PAKISTAN LAKINI WAKUMBUKE HADI 1936 ZANZIBAR NA INDIA(INDIA NA PAKISTAN)ZILIKUA MAKOLONI YA KINGEREZA HIVYO MOVEMENT ZA BIDHAA ILIKUA HAINA VIKWAZO NA SOTE TULIKUA TUNATUMIA RUPIA.

    HAYA LEO HII, NAATOKE HAPA HUHADIMU AKANUNUE TENA MBAO INDIA TUONE BEI YAKE?..HIYO FREIGH TUU UTAJUTA!

    ZAIDI YA YOTE HAYO, LAKINI NA TANGANYIKA NAO WANATUMIA MPASUKO WETU WA KIJAMII NA NJAA KUTUUMIZA,

    KUMBE KUNA GAWIO LA BENKI KUU, KODI ZA WAFANYAKAZI WA SEKTA ZA MUUNGANO, NAFASI ZA MABALOZI, GESI YA SONGO SONGO AMBAYO IMEGUNDULIWA BAADA YA MUUNGANO KIMYAAA!! HATUPATI MAELEZO!
    AU KAMA CHUO KIKUU CHA DSM MIAKA YOTE HII WAMESHINDWA HATA KUFUNGUA KAMPAS HAPA, WAKATI ELIMU YA JUU NI MAMBO YA MUUNGANO..HEBU TUJIULIZE JAA, TATIZO NI WABARA AU WATU WETU?

    ReplyDelete
  11. Zanzibar ilikuwapo kabla ya muungano na itaendelea kuwepo kwa uwezo wa mungu baada ya kuondoka kwa huo muungano wa dhulma. Amani ilikuwepo Zanzibar kabla ya Muungano na itaendelea kwa uwezo wa mungu kuwepo baada ya kuondoka huo muungano wa dhulma.

    Waliotuunganisha ni hao hao walioleta dhulma na mauaji mnayoyaita mapinduzi ambapo maelfu ya wazanzibari walidhulumiwa roho zao na wakafa mashahidi. Waloleta balaa la mapinduzi (mauaji) ndiyo waloleta nakama ya muungano!

    Bilal usikubalia kuuza heshima yako kwa thamani ndogo ya maslahi. Maneno yako hayana nguvu tena! na kwa kutumia maneno ya hamad rashid usiwe political prostitute.

    ReplyDelete
  12. Na kama Z'bar yenyewe muitakayo ni hiyo ya kuja kuwalipizia visasi wazee wetu kwa kufanya mapinduzi basi mjue hamtafanikiwa!..tutakwenda hivi ..hivi!
    Mungu ibariki Z'BAR..Mungu ubariki muungano..Mapinduzi daimaa!!!

    Yaani mimi nlizani tumebadilika,tumesahau yaliyopita baada ya takriban miaka 48, tuna serikali ya umoja wa kitaifa, Allah ameanza kufungua neema zake baada ya "kubadilisha yale yaliyokua ktk nyonyo zetu" ..kumbe bado?..yaani dhulma inatajwa ya upande mmoja tuu?

    Ama kweli..ni kutu la ng'ombe juu kavu, chini bichi!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.