Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohamed alisisitiza suala la matunzo ya watoto pamoja na kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsi kwamba vimepewa kipaumbele katika utekelezaji wa Wizara hiyo kwa mwaka huu 2012-2013.
Zainab alisema hayo wakati ujumbe wa Wizara hiyo ulipokutana na rais wa Zanzibar dk.Ali Mohamed Shein Ikulu katika utaratibu wa kukutana na watendaji wa wizara mbali mbali za Serikali kujuwa utekelezaji na mipango kazi waliyojipangia.
Alisema suala la vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji vimepewa kipaumbele,ambapo Elimu kwa jamii inahitaji ili kuona watu wanaachana na ukatili huo kwa watoto.
'Tumejipanga kuona kwamba kasi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya watoto chini ya umri wa miaka 15 vinaondoka moja kwa moja'alisema.
Aidha alisema lipo tatizo kubwa katika jamii kwa watoto kufanya kazi ngumu bila ya ridhaa yao kwa ajili ya kupata Fedha.
Alisema tatizo hilo kwa kiasi kikubwa limewafanya watoto kukosa moja ya haki yao ya msingi ambayo ni Elimu kwa maendeleo ya taifa.
Mapema dk.Sheni alisema amefurahishwa na mikakati hiyo ya kazi kwa Wizara ya wanawake na watoto kwa mwaka 2012 ambayo inakwenda sambamba na malengo ya mikataba ya kimataifa ya kukomesha ajira kwa watoto.
'Ni mipango mizuri na nimeridhika nayo moja kwa moja...ipo haja kubwa ya kupambana na ajira za watoto ambazo zinarudisha nyuma juhudi za taifa la kuwapatia watoto Elimu ya msingi;'alisema Sheni.

No comments:
Post a Comment