UELEWA mdogo walionao wananchi juu ya mfumo wa mahakama na jinsi inavyotekeleza majukumu yake, ni moja ya sababu zinazochangia jamii kunyimwa haki zao na kushindwa namna ya kuzitafuta haki hizo.
Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi aliyasema hayo jana mjini Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akielezea maadhimisho ya siku ya sheria Zanzibar.
Alisema kutoeleweka kwa mfumo wa mahakama na ni miongoni mwa kikwazo kinachochangia jamii kukosa haki zao mahakamani na kutojua fursa ya kutafuta haki kwa muda na mahali muafaka.
Alifahamisha kuwa mbali na changamoto hiyo, pia jamii imejenga dhana kuwa mahakama ni sehemu iliyowekwa maalum kwa watu maalum na yeyote anayekwenda mahakamani basi huishia jela.
“Wananchi wengi Zanzibar bado hawaelewi vyema kazi za mahakama na hivyo kuwa na dhana kwamba mahakamani ni sehemu ya watu wa aina fulani tu, na yeyote anayekwenda mahakamani basi ataishia jela”,alisema Mrajis huyo.
Alifahamisha kuwa dhana hizo potofu ambazo wananchi wanazo ndani ya vichwa vyao, zinatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya kazi na majukumu ya mahakama.
Aidha alisema matatizo hayo yaliyopo katika jamii ya ufahamu mdogo wa mahakama kwa kiasi kikubwa yanachangia wananchi kujichukulia sheria mikononi mwao.
Mrajis huyo alisema suala la kujichukulia sheria mikononi ndilo linalochangia kutendeka kwa makosa zaidi ama ya jinai au madai kwa watu kuwapiga hadi kuwaua wezi au kuharibu mali na kusababisha kuibuka kwa migogoro katika jamii.
Hata hivyo alifahamisha kuwa siku ya sheria wataitumia kutoa elimu kwa jamii juu ya uwepo wa mahakama na kazi zake mbali mbali katika utoaji wa haki kwa jamii.
Kazi alisema kuwa vyombo vya Habari vina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii katika zoezi zima la kutoa elimu kwa jamii kuhusu mahakama inavyofanya kazi zake na jinsi itakavyoweza kuwapatia haki wananchi kwenye matatizo yao mbali mbali.
Alitoa wito kwa mahakimu mbalimbali kuwa makini juu ya hukumu zao wanazozitoa zikiwa na ukweli na zenye uchunguzi zaidi.
Pia aliwataka waepukane na rushwa kwani kumekuwa na tabia ya mahakimu kuwa wanapokea rushwa na ndio maana hawafanyi haki za kutoa hukumu.
Maadhimisho hayo ya siku ya sheria Zanzibar inatarajiwa kufanyika Februari 7 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa

No comments:
Post a Comment