Habari za Punde

Zoezi la Upigaji Kura Uchaguzi Mdogo Uzini.

Mwananchi akipiga kura katika Kituo cha skuli ya Uzini kumchagua Mwakilishi amtakae katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini.
Karani wa Kituo cha Upigaji kura katika skuli ya Uzini akimkabidhi kura yake Mwanchi aliefika kituo hapo kupiga kura ya kumchaguwa Mwakilishi wake wa Jimbo la Uzini.
Ofisi Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ali Rashid Suluhu, akizugumza na Waandishi wa habari jinsi zoezi la Upigaji kura linavyoendelea katika vituo mbalimbali.akiwa katika Kituo cha Skuli ya Mgenihaji.
Mawakala wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini, wakiagalia majina ya Wapiga Kura katika Kituo cha Banda la Karafuu Keboje Muembeshauri.  
Mwananchi akipiga kura yake katika Kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Kiboje.
Karani wa Kituo cha kupigia Kura cha Kiboje Muembeshauri, akiwaweka wino maalum Wananchi waliokwishapiga kura katika kitio hicho.  
Karani wa Kituo cha Upigaji Kura akipiga muhuri karatasi ya Kura.
Mwananchi akiagalia jina lake katika Kituo cha Skuli ya Kiboje, wakati wa zoezi la Upigaji kura likiendelea katika jimbo la Uzini. 
Mwananchi akipiga kura yake kutimiza haki yake ya msingi kumpigia kura mtu amtakae  


Mawakala wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini wakizungumza na Waandishi wa Habari jinsi zoezi linavyoendelea katikac kituo chao cha Skuli ya Uzini.
Mwananchi akiagalia jina lake katika kituo cha Skuli ya Uzini.
Katibu Mkuu wa Chama cha TADEA Ali Juma, akizungumza na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar Leo maendeleo ya Uchaguzi Mdogo wacJimbo la Uzini, unavyoendelea kwa Amani na Huru, akiwa katika kituo cha Skuli ya Mchangani.    
Mgombea Uwakilishi katika Jimbo la Uzini kupitia Chama cha AFP Rashid Mchenga, akizungumza na Mwandishi wa habari wa gazeti la Zanzibar Leo Mwantanga Ame, katika kituo cha Skuli ya Mchangani.
Viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini, CCM na TADEA wakibadilishana mawazo, wakati zoezi likiendelea katika vituombalimbali vya Uchaguzi katika Jimbo la Uzini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.