Na Mwashamba Juma
WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud,
amesema harakati za mwanadamu kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikichangia kubadilika kwa mfumo wa hali ya hewa ambayo yanaathiri mazingira.
Alisema kuna viashiria kadhaa ulimwenguni ambavyo vyengine vimesababisha na shughuli za binaadamu vinavyoonesha ni matukio mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari, kuyeyuka kwa theluji na barafu.
Waziri huyo alieleza hayo jana kwenye hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duniani, yaliyofanyika katika kiwanja cha Ndege cha Zanzibar .
Alisema kuongezeka kwa kasi ya majanga asilia, yanayoathiri mfumo mzima wa maisha ya watu ulimwenguni kote kunatokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande mwengine, waziri huyo aliwataka wananchi kutodharau taarifa zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kwenda sambamba na mabadiliko ya tabia nchi na kuepukana na athari za majanga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kanda ya
Akizitaja changamoto zinazoikumba Mamlaka hiyo ni pamoja na upungufu wa vituo na vifaa vya kupimia hali ya hewa, upungufu wa wataalamu ambao unatokana na wengi wao kustaafu.
Naye Bakari Mussa kutoka Pemba, anaripoti kuwa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Karume Pemba, Amour Mussa Makame amesema uchafuzi wa mazingira unaofanywa na binaadamu mwenyewe unachangia mabadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumza na wanafunzi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani, alisema uchafuzi wa mazingira ni moja ya changamoto zinazoikabili hali ya hewa hasa uzalishaji wa hesi joto.
Naye Meneja wa Mamlaka ya hali ya Hewa Pemba, Salim Ismail Kanduru, alisema kuwa huduma za hali ya hewa ni muhimu katika kuepuka majangana na ni matokeo mazuri ya hatua yanategemea jamii iliyojiandaa vyema kukabiliana na changamoto hizo.
Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani hufanyika kila mwaka Machi 23, ambapo ujumbe wa mwaka huu ni “Hali ya Hewa na Maji kwa mustakabali wetu”.
No comments:
Post a Comment