Habari za Punde

Zanzibar yatiliana Saini na China Ujenzi wa Skuli

Na Mwantanga Ame

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya amali imetiliana saini na serikali ya China mkataba wa ujenzi wa skuli ya msingi huko Mwanakwerekwe.

Utiaji saini huo ulifanyika juzi kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Abdulla Mzee Abdulla  na Meneja wa kampuni ya Fujian Cosrtuction Engineering Group Cooporation, kutoka China, Huang Mei Luan.
Mkataba huo umekuja ikiwa ni msaada wa serikali ya China baada ya kujitolea kuipatia Zanzibar Yuan milioni 15,000,000 ambazo sawa na dola za kimarejani milioni 1.5.

Utekelezaji wa mkataba huo unatarajiwa kuanza Aprili mwaka huu ambapo skuli hiyo itajengwa katika eneo la Mombasa mkabala na Mwanakwerekwe.

Baada hya kutia saini mkataba huo, Naibu Katibu Mkuu huyo aliishukuru kampuni hiyo na kuiomba kutekeleza sawa sawa mkataba huo kwa kufuata wakati kukamilisha kazi hiyo.

Alisema suala la kufuata wakati ni moja ya jambo la msingi kwani litaisaidia serikali kupunguza matatatizo inayoyakabili katika sekta hiyo ya kupata majengo ya kupata elimu.

Nae Meneja wa Kampuni hiyo aliishukuru serikali ya Zanzibar na kuahidi kutekeleza masharti ya mkataba huo kma ilivyokubaliwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.