Na Madina Issa
WANANCHI wa
Katibu Mkuu wa wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati Mwalim Ali Mwalim aliyasema hayo alipokua akizungumza na wanajumuiya wa hifadhi ya mazingira Kikobweni na wananchi wa kijiji hicho wakati wa upandaji wa miti, iliyopandwa pembezoni mwa mto, ikiwa ni shamrashamra ya juma la wiki ya maji duniani.
Alisema endapo wananchi watavitunza vianzio hivyo wataweza kuepukana na ukosefu wa maji kwa vile vianzio ndio chanzo cha kupata maji safi na salama.
Aidha alisema kuwa maji ni muhimu na yanahitaji kuhifadhiwa hivyo wananchi wanatakiwa kuhifadhi vianzio hivyo ili kuepusha upotevu wa maji na kupelekea usumbufu kwa wananchi wengi.
Sambamba na hayo aliwataka wananchi wahakikishe wanayadhibiti maji kwa kutoyaacha yakimwagike ovyo katika majumba
Hata hivyo aliwapongeza wanajumiya hiyo kwa kuweza kutunza mto huo ambao unaonekana wenye haiba ya kupendeza na usafi wa hali ya juu zaidi na kuweza kutumiwa na wananchi wengi ambao wapo
katika kijiji hicho.
Akisoma risala Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Mazingira Kikobweni, Mwanaisha Makame Abdalla alisema jumuiya
Aidha waliwaomba wahisani na wafadhili kuwapatia mafunzo ya uhifadhi wa mazingira pamoja na uhuifadhi wa vyanzo wa maji kwani hivi sasa wanmekuwa wanafanya kazi zao bila ya elimu yoyote.
Jumuiya hiyo imeanzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanachama 30 ambapo iliwahi kufadhiliwa na Tasaf na wameweza kupatiwa mradi wa upandaji wa miti katika vianzio vya maji pamoja na kusafisha mazingira.
Katika mto huo jumla ya miti 20,700 aina tofauti tayari ilipandwa pembezoni mwa mto huo ikiwemo michikichi,mibuyu maji , mifenesi, michaichai, mibungo, miudiudi, mipopoo, mitondoo, mikungu na mibambakofi.
No comments:
Post a Comment