Na Rehema Abdulrahman, MCC
KATIBU wa kikundi cha ushirika cha Imani Sieni, Khamis Salum amewataka wanachama wa kikundi hicho kujenga tabia ya ushirikiano katika kazi zao ili wapate kusaidiana pia kuondokana na ukali wa maisha.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi huko ofisini kwake, Kombeni kichungwani wilaya ya Magharibi Unguja.
Sieni alisema ili kuepukana na ukali wa maisha, uliopo hivi sasa nchini ni vyema wanakikundi hicho wakaweka tabia ya ushirikiano wa kazi zao katika kuhakikisha wamepiga hatua za kimaendeleo zitakazowasaidia kimaisha.
Aidha alisema kikundi cha ushirika cha Imani kimeanzishwa 2010 na hujishuhulisha zaidi na kuweka na kukopa pesa, na kwa sasa kina jumla ya wanachama 30 ikiwa ni pamoja na wanawake 28 na wanaume 2.
Hata hivyo alieleza kuwa faida inayopatikana katika kikundi hicho ni kupata kujikwamua katika matatizo madogo madogo ya kifamilia ambapo ni pamoja na kununulia sabuni, kulipia watoto ada za maskuli pamoja na chuoni.
Pia amewaomba wajitolee kufanya kazi za kujiajiri wao wenyewe baadae na kuondokana na dhana ya kutegemea kupata ajira Serikali hali ambayo imekuwa ngumu
Pamoja na hayo Sieni alitoa wito kwa kinababa kutumia fursa ya kujiunga katika vikundi hivi vya ushirika kwani havina jinsia moja bali vinaweza vikapata manufaa pakiwemo na pande zote mbili za jinsia ikiwemo wanawake na wanaume.
Aidha alitoa ushauri kwa wanakikundi hicho kuweza kujishuhulisha katika kazi kikamilifu na kutumia jitihada zao kikazi ili kujiimarisha na kupata kipato kitakachokidhi mahitaji
Nao wanakikundi cha ushirika walisema kuwa endapo Serikali itajitolea kusaidia kila kikundi cha ushirika
No comments:
Post a Comment