Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, akitoa taarifa ya kifo cha Mwakilishi wa Bububu Salum Amour Mtondoo, baada yackupata taarifa akiwa katika Mkutano wa Uvuvi Haramu Ukumbi wa Zanzibar Beach Mazizini leo asubuhi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akizungumza na waandi nje ya ukumbi wa mkutano, baada ya kufungua semina hiyo na kutowa wasifu wa marehemu wakati wa uhai wake katika kuchangia katika kikao cha baraza na kusema ameacha pengo kubwa barazani.
Waheshimiwa wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi mmoja wakitafakari kifo cha mwakilishi mwezao marehemu Salum Amour Mtondoo, kilihotokea katikqa hospitali ya Mnazi Mmoja katika wodi ya ICU saa nne leo.
Mbunge wa Jimbo la Bububu Sururu, akiwa na majonzi ya kifo cha mwakilishi wa jimbo hilo wanaloliongoza baada ya uchaguzi wa mwaka juzi, akitowa taarifa kwa jamaa akiwa nje ya wodi ya ICU.
Mwili wa marehemu Salum Amour Mtondoo, mwakilishi wa Jimbo la Bububu ukichukuliwa katika hospitali ya Mnazi mmoja ili kupelekwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa kutoa heshima ya mwisho na kuangwa na Wajumbe.
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi wakiubeba Mwili wa Marehemu Salum Amour Mtondoo wakiuigiza katika ukumbi wa baraza kwa kutoa heshima na kuuombea dua.
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi wakiubeba Mwili wa Marehemu Salum Amour Mtondoo wakiuigiza katika ukumbi wa baraza kwa kutoa heshima na kuuombea dua.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Alhaj Fadhi Soroga akitowa duwa wakati wa kuuombea mwili wa marehe Salum Amuor Mtondoo, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kutowa heshima na kuuaga.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiitikia dua wakati wa kuuombea mwili wa marehemu Salum Amour Mtondoo, Mwakilishi wa Bububu, ulipoletwa ukumbi wa baraza kutowa heshima za mwisho.
Waheshimiwa Wawakilishi wakiwa na majonzi ya kuondokewa na Mwakilishi Mwezao wa Jimbo la Bububu Salum Amour Mtondoo.
hili suala la kupeleka maiti barazani sijui ata nani alielisnshisha ila ila halileti picha nzuri kabisa na hasa kwa sisi waislamu.
ReplyDeletemdau wa juu nakuunga mkono maana hata mimi sipati picha naona tunazidi kuongeza mambo yasiyohusu katika jamii
ReplyDelete